Tuesday, January 12, 2021

Mwanamitindo Naomi Campbell atangazwa kuwa balozi wa Kenya wa Utalii




Mwanamitindo Naomi Campbell amekubali uteuzi wa kuwa balozi wa kimataifa wa Utalii Kenya.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utalii na Wanyamapori, makubaliano hayo yamefikiwa kati ya Campbell na waziri wa utalii na wanyamapori, Najib Balala.

"Tunafurahishwa na taarifa kuwa Naomi Campbell atakuwa balozi wa utalii na kusafiri kimataifa akitangaza Kenya" Waziri amesema.

Wakati wa mkutano huo, Naomi Campbell alisifu serikali ya Kenya kwa kuimarisha miundombinu katika eneo la pwani ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwanja wa ndege wa Malindi kuwa wa hadhi ya kimataifa na kuongeza kuwa hatua hiyo itaimarisha utalii katika eneo hilo.

Mwanamitindo huyo maarufu duniani atasaidia kuitangaza Kenya kama eneo ambalo ni kivutio cha utalii duniani.

Bi Campbell amekuwa  akitembelea mara kwa mara eneo la Malindi kuvinjari nyakati za mapumziko yake.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...