Wednesday, January 13, 2021
Fisi Azua Taharuki Shinyanga..... Ajeruhi Mzee Wa Miaka 70 Na Mwanae wa Miaka 17
SALVATORY NTANDU
Wakazi wawili wa Kijiji cha kilimawe kata ya Mwantini mkoani Shinyanga, Mabuga Ndakuna (70) na Timotheo Mabuga ( 17) wamejeruhiwa na mnyama aina ya fisi wakati wakijaribu kuokoa mifugo yao iliyokuwa kwenye banda la nyumba yao isishambuliwe na mnyama huyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana na kusema kuwa tukio hilo limetokea Januari 11 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri ambapo fisi huyo alivamia banda la kuku katika familia ya Mzee Mabuga na kushambulia kuku ndipo katika harakati za kumfukuza alianza kuwashambulia.
"Mzee Mabuga Ndakuna aling'atwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani,miguuni na kuvunjwa mkono wa kushoto huku mwanae Timotheo aking'atwa sehemu mbalimbali za mwili wake kama vile mikono,miguuni na mabegani,"alisema Magiligimba.
Kamanda Magiligimba alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni mnyama huyo aina ya fisi kuvamia banda la kuku na wanafamilia hao kutoka nje kwenda kuokoa mifugo yao isiendelee kushambuliwa ambapo baada ya kutekeleza tukio hilo alikimbilia vichakani.
"Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, hali zao zinaendelea vizuri na jitihada za kumtafuta mnyama huyo zinaendelea ili kuwaondoa wanyama wakali katika kijiji hicho kwa kushirikiana na maafisa wanyama pori,"alisema Magiligimba.
Mwisho.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
