Saturday, January 2, 2021

Daktari wa Kituruki aboresha kifaa cha Covid-19




Daktari wa Kituruki ameunda kifaa maalum cha kuhifadhia mkojo kwa ajili ya kugundua aina mpya ya virusi vya corona (Covid-19).
Mtaalam wa Physiotherapy Dr. Mehmet Serhan Kurtulmuş ameunda kifaa cha uhifadhi ambacho asidi ya amino na miundo ya viini vya protini maalum katika virusi vya Sars Cov-2, vinaweza kugunduliwa kwenye mkojo.

Kurtulmuş alisema katika taarifa juu ya kifaa kilichotengenezwa kwamba alianzisha shughuli ya uboreshaji mnamo mwezi Machi baada ya Covid-19 kuonekana kwa mara ya kwanza nchini Uturuki, na matokeo yake yakapatikana mwezi Novemba.

Kurtulmuş aliongezea kusema kuwa kabla ya majaribio ya kifaa hicho, kwanza ilipitishwa na Wakala wa Dawa na Vifaa vya Tiba nchini Uturuki, na baadaye ikaidhinishwa na Idara Kuu ya Usimamizi wa Afya ya Umma, na kwa sasa pia kimeruhusiwa na Wizara ya Afya.

Akisema kuwa kiwango cha usahihi cha jaribio ni kikubwa kuliko vipimo vilivyopo katika utafiti wa kliniki uliofanywa kwa idhini ya kamati ya maadili, Kurtulmuş alisema kwamba utafiti huu ulichapishwa kwenye jarida la kliniki kimataifa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...