Monday, January 11, 2021

BI. HARUSI AFARIKI DUNIA GHAFLA BAADA YA KUTOKA FUNGATE

Linet 
Mnamo Disemba 11, 2020, Mastin Mukanga alifunga pingu za maisha na Linet Kavere katika harusi maridadi lakini bibi harusi aliaga dunia siku 18 baadaye.

Wawili hao walikutana katika Chuo Kikuu cha Masinde Muliro wakiwa wanafunzi na kuanza kuwa marafiki wa dhati na kisha baadaye kuchumbiana baada ya kumaliza chuo.

 Mastin alipata ajira kama Mhandisi katika Shule ya Msingi ya Phanero mjini Mbale huku Linet akipata nafasi ya kufunza Kizungu katika Shule ya Wasichana ya Mbihi. 

 Waliidhinishwa rasmi kuwa mume na mke kwenye harusi iliyoandaliwa katika bustani la Sosa, Disemba 2020. 

Wakati wanandoa hao walirejea kutoka kwa fungate yao, walikuwa wanaazimia kuishi maisha ya raha mstarahe hadi kifo kitakapowatenganisha.

 Lakini walitenganishwa siku moja baada ya fungate huku Linet akianza kukumbana na matatizo ya kupumua, akazirai na kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Kisumu Specialists ambapo alithibitishwa kufariki saa chache baadaye. 

Humphrey Odanga, mwalimu mkuu wa Mbihi, ambapo marehemu alikuwa akihudumu, alimsifu Linet kwa kuwa mwalimu mwenye bidii. 

"Alikuwa nasi karibia miaka miwili na kando na kuugua magonjwa ya kawaida kama mtu yeyote yule, hakuonyesha dalili zozote za kuwa na changamoto za kiafya," alisema. 

Kulingana na Bi. Jane Ambani, rafiki wa familia hiyo, kifo chake cha ghafla kiliwashtua wengi.

 "Bibi harusi hata hakuwa ameanza kuishi kwa nyumba ya bwana harusi ya Magada tangu harusi yao," alisema.

 Linet alizikwa Jumamosi, Januari 9, 2021, saa tatu baada ya mwili wake kuwasili kutoka makafani kulingana na sheria za COVID-19.

 Matokeo ya upasuaji ilionyesha kuwa Linet alikumbana na shinikizo la damu kwenye mishipa. 

Wafanyakazi wenzake pamoja na marafiki zake walitoa rambi rambi zao kufuatia kifo chake.

CHANZO - TUKO NEWS


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...