Uswisi imekuwa nchi ya kwanza kuidhinisha chanjo iliyozalishwa na Pfizer na BioNTech katika taratibu za kawaida.
Katika taarifa iliyotolewa na taasisi inayosimamia sheria katika kitengo cha matibabu na afya nchini Uswisi Swissmedic, ilielezwa kuwa data zilizopatikana kutoka kwa watu wa umri mbalimbali zilionyesha kuwa chanjo inakidhi mahitaji ya ufanisi na usalama. Taarifa hiyo pia ilisisitiza kuwa chanjo ilipitishwa chini ya taratibu za kawaida, wala sio kwa matumizi ya dharura, na hii ilikuwa ya kwanza ulimwenguni.
Mkurugenzi wa Swissmedic Raimund Bruhin, alibaini kufanya ukaguzi kwa uangalifu wakati wa mchakato wa kuidhinisha na kusema kuwa chanjo iliyozalishwa na Pfizer na BioNTech inakidhi vigezo vya usalama, ufanisi na ubora.
Uswizi imeagiza jumla ya dozi milioni 15.8 za chanjo ya Covid-19 iliyozalishwa na Moderna na AstraZeneca, pamoja na chanjo ya Pfizer na BioNTech.
Waziri wa Afya wa Uswisi Alain Berset alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter na kusema kwamba chanjo itaanza kutolewa ndani ya siku chache. Barset pia alisisitiza kuwa chanjo hiyo itatolewa bure na kupendekeza matumizi yake.
Kulingana na mpangilio uliopo, chanjo hiyo inatarajiwa kuanza kutolewa kwa awamu ya kwanza ya dozi 100,000 kuanzia Januari 4. Kampeni hiyo ya chanjo itaendelea na watu milioni 6 wanatarajiwa kufanyiwa chanjo ifikiapo msimu wa joto.