Sunday, December 20, 2020

Rais wa Mexico na Biden waahidi kujenga uhusiano

 


Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador amefanya mazungumzo ya kwanza kwa njia ya simu na Rais Mteule wa Marekani Joe Biden, ikiwa ni baada ya rais huyo kutoa pongezi zake mapema wiki hii. 

Lopez Obrador aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, jana, Jumamosi " Tumejizatiti katika jukumu la kufanya kazi pamoja kwa ustawi wa watu wetu na mataifa yetu." 

Lopez Obrador alimpongeza Biden, muda mfupi baada ya Wajumbe wa jopo la Uchaguzi wa Marekani kuthibitisha ushindi wake mapema juma hili, ikiwa ni zaidi ya siku 40 baada ya kumalizika uchaguzi wa Marekani wa Novemba 3. 

Lakini pia rais huyo aliweza kujenga uhusiano na rais wa sasa wa Marekani Donald Trump licha ya ahadi yake ya kujenga ukuta katika eneo la mpaka wa kilometa 3,200 kati ya Marekani na Mexico.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...