Thursday, December 17, 2020

Misafara ya kwanza ya msaada yawasili jimboni Tigray, Ethiopia

 


Misafara ya magari yaliyobeba msaada wa kibinadamu imeanza kuwasili katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, ambalo lilikuwa katika mzingiro wakati wa vita baina ya vikosi vya serikali kuu na chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF kinacholiongoza jimbo hilo. 

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema misafara hiyo iliwasili jana ikiwa na maelfu ya tani za vyakula, na kuongeza lakini kuwa bado hali sio ya kuridhisha.

Dijarric amesema malori ya Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP yalipeleka tani 570 za chakula, yakielekea katika kambi za wakimbizi wa Eritrea za Adi Harush na Mai Ayni, ambazo zinatosha kuwalisha kwa mwezi mzima watu 35,000. 

Amesema misafara mingine ya msaada itaondoka baadaye kuelekea katika kambi nyingine.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...