Monday, December 21, 2020

Jafo Ataka Wakurugenzi wa Halmashauri Nne Kujieleza



Waziri JafoWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo leo Desemba 21, 2020 ameagiza wakurugenzi wa halmashauri nne za Msalala, Kahama, Korogwe na Sikonge, kutoa maelezo kwa nini hawakuwaruhusu walimu kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa).

 

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa umoja huo leo jijini Dodoma na kueleza kuwa serikali ilitoa kibali cha mkutano huo kwa sababu wanaamini malengo makuu ya kiserikali yatawafikia walengwa wanaohudhuria lakini wakurugenzi hao walishindwa kutoa kibali kwa walimu husika kwenda kupata maelekezo ya serikali.

 

"Anatokea mkurugenzi anakataa kutoa kibali kwa hawa wapiganaji wa Dk John Magufuli… namuagiza katibu mkuu apate maelezo ya hawa," alisema Jafo akitaka jambo hilo lifanyike mara moja.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...