Wednesday, June 3, 2020

Maandamano nchini Argentina kukemea mauaji ya George Floyd




Maandamano kupinga mauaji ya George Floyd yaendelea kufanyika katika mataifa  tofauti ulimwenguni. 

Maandamano kukemea mauaji ya mmarekani mweusi George Floy, mtu mweusi aliefariki akiwa mikononi mwa polisi. 

Floyd amefariki wiki iliopita wakati amekamatwa na polisi, afisa mmoja wa jeshi la Polisi alimkandamiza kwa goti shingoni kwa muda wa dakaki kadhaa na kufariki. 

Mjini Buenos Aires nchini Argentina, mjini kati  wamekusanyika mwaandamanaji walionesha ghadyhabu zao dhidi ya matumizi ya kukithiri ya nguvu dhidi ya  watu weusi pindi wanapokamatwa nchini Marekani. 

Waandamanaji wamedai haki itendeke kwa George Floyd. 

Waandamanaji hao waliokuwa pia wakitoa kauli  dhidi ya rais wa Marekani Donald Trump. 

Kufuati kifo cha George Floyd Mei  25, maandamano ya ghasia na uporaji vimeshuhudiwa katika miji tofauti nchini Marekani.

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...