Njia za ueneaji wa ugonjwa huu.
Utupaji ovyo wa mizoga ya kuku, kwani mzoga unaweza kukaa na vimelea kwa zaidi ya miezi mitatu.
Kupitia chakula na maji yenye mchanchanyiko na vimelea hivyo.
Kuku mzima kugusana na kuku mgonjwa.
Kupitia njia ya upumuaji.
Dalili za ugonjwa huu.
Huarisha majimaji ya kijani yenye harufu.
Kilemba na masikio ya kuku hupauka na kulegea.
Hupumua kwa shida.
Hutokwa na ute mdomoni na puani.
Joto la mwili hupanda.
Vifo hutokea
Jinsi ya kuthibiti ugonjwa wa fowl cholera.
Usafi wa ndani na nje ya banda.
Tenganisha kuku kwa rika zao (wakubwa kwa wakubwa na wadogo kwa wadogo).
Zingatia sifa za banda bora.
Mizoga ichomwe moto au ifukiwe katika shimo la kina kirefu kuzuia kuenea kwa ugongwa.
Tiba ya fowl cholera.
Ukiona dalili za ugonjwa huu wahi mapema kutumia dawa mojawapo kati ya zifuatazo:~
Trimazin
Typhoprim
Sulphonamides
Hipraloma
O.T.C
C.T.C
Ganadex
Source