Saturday, April 18, 2020

Mvua yasababisha kifo Dsm

Msichana Mmoja anayekadiliwa kuwa na Umri wa Miaka 15 au 16 amefariki Dunia baada ya nyumba yao kuangukiwa na Jiwe kubwa lililosababishwa na Mmomonyoko wa Udongo kutokana na Mvua Kubwa zinazoendelea kunyesha katika Mtaa Makangira Msasaji jijini dsm.

Mmomonyoko wa Udongo na Kuanguka kwa jiwe hilo kunatokana na Kufurika kwa Maji katika eneo hilo la Msasani ambako pia kunatishia kufumuka kwa bomba kubwa la dawasa linalopeleka Maji Masaki lakini pia nyumba nyingine tatu zipo hatarini kuanguka.

Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta alifika katika eneo hilo kwa ajili ya kutoa Pole na kuutaka Uongozi wa Mtaa huo kuhakikisha Kuwa wakazi waliobaki ambao nyumba zao ziko hatarini kuondolewa ili kuepuka Maafa mengine yanayoweza kutokea.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...