Friday, April 17, 2020

Italia bado haijaweza kurejesha shughuli za kawaida za maisha

Wakati Ujerumani ikitangaza kwamba mripuko wa kirusi cha corona sasa umedhibitiwa na kuamuru kuanza kurejea kwa shughuli za kawaida za maisha kuanzia tarehe 4 mwezi ujao, huenda hali nchini Italia ikasalia kama ilivyo kwa kipindi kirefu kijacho.

Waziri wa Elimu wa Italia, Lucia Azzolina, amesema kutokana na hali ilivyo hadi sasa, hakuna uwezekano wa kufunguliwa kwa shughuli zozote mwezi Mei.

Akizungumza na gazeti la Corriere della Sera hivi leo, waziri huyo amesema hawawezi kubahatisha kuwatoa wanafunzi milioni nane kuingia mitaani kwa sasa.

Italia ndilo taifa la Ulaya lililoumizwa sana na janga la COVID-19, likiripoti vifo zaidi ya 22,000 na maambukizi yakaribiayo 170,000.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...