Wednesday, July 3, 2019

Ununuzi wa zao la Pamba wilayani Kahama wafanyika kwa kusuasua licha ya soko lake kufunguliwa May 5 mwaka huu.

NA SALVATORY NTANDU
Makampuni yaliyopewa leseni za kununua zao la pamba katika wilaya ya kahama mkoani Shinyanga yametakiwa kununua zao hilo kwa wakulima kwa wakati ili kutoa fursa ya maandalizi ya msimu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Emmanuel Kileo Mkaguzi wa Pamba wilaya ya kahama wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana namna soko la zao hilo linavyoendelea baada ya kuzinduliwa may 5  mwaka huu.

Amesema kampuni nne zilizopewa leseni ya kununua zao hilo zimekuwa zikinunua zao hilo kwa kusuasua  na kusababisha wakulima wengi kulalamikia namna masoko ya zao hilo unavyofanyika na yanatakiwa kununua kwa bei elekezi ya shilingi elfu moja na mia mbili.

Amefafanua kuwa mpaka sasa kampuni mmoja pekee ya Fresho ndio imeweza kununua pamba za wakulima kwa kiwango kidogo huku makampuni mengine yakiwa hayajaanza ununuzi wa lincha ya msimu wa zao hilo kuzinduliwa.

"Wakulima wetu wamehamasika kulima zao hili na mwaka huu tunatarajia kupata kilo milioni 4 na laki saba ilikiganishwa na mwaka jana ambapo walilima kilo milioni 2 na laki tatu"alisema Kileo.

Hata hivyo Kileo amesema kwa ukaguzi ambao ofisi yake imeufanya wamebaini pamba yote ni safi na haijachanganywa na maji na kuwataka wakulima kuzingatia sheria na taratibu za utunzaji wa zao ili ili kupata manufaa zaidi wanapoifikisha sokoni.

Kampuni ambapo zimepewa  leseni hizo ni pamoja na Fresho, kahama oil mills, Kahama Cotton Company Limeted na Africian lakini kampuni ya fesho ndio imeweza kununua pamba pekee ambapo imenunua katika vijiji 46 kati ya 148 vinavyolima zao la Pamba.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...