Mtu mmoja aliyesadikia kuwa ni jangili wa wanyama aina ya faru ameuawa na Tembo kisha kuliwa na Simba katika hifadhi ya taifa ya Kruger, nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mamlaka ya utafiti nchini humo, baada ya uchunguzi imeweza kugundua fuvu pamoja na masalia ya nguo ya mtu huyo.
Pia Mamlaka ya Hifadhi za Taifa nchini iliseme Ijumaa kuwa jangili huyo pamoja na washirika wenzake wanne walikuwa wakijaribu kuwinda wanyama aina ya faru, jioni ya Jumanne, ambapo washirika hao waliiambia familia ya marehemu kuwa mwenzao ameuawa na Tembo.
Mkurugenzi wa hiadhi hiyo ametoa salamu za rambirambi kwa familia huku akitoa angalizo kuwa, ''kuingia kwenye mbuga ya Kruger kinyume cha sheria na kwa miguu si jambo jema,'' alisema Murugenzi huyo. ''ni mbuga yenye hatari nyingi na tukio hili linadhihirisha hayo''.
Hifadhi ya Kruger imekua ikikabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe za faru kwenye nchi za bara la Asia.
Nchi ya Afrika Kusini ina takribani faru 20,000, ambayo ni asilimia 80 ya faru wote wanaopatikana dunia nzima. Tangu mwaka 2008, jumla ya faru 7,000 wamewindwa kinyume na utaratibu nchini humo, ambapo 1028 kati yao wakiuawa katika mwaka 2017 pekee.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumk...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...
-
Wanajeshi wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa baada ya kifaru cha Israel kufyatua risasi kuelekea mnara wa Umoja wa M...