Monday, August 6, 2018
Wachezaji wa Simba waikubali Coastal Union
Wachezaji wa Simba waliotolewa kwa mkopo kwenda Coastal Union ya Tanga, Moses Kitandu na Haji Ugando wameeleza kuridhishwa na mwenendo wa mazoezi chini ya kocha Juma Mgunda huku wakiahidi kuwa wapo tayari kujitoa kwaajili ya timu hiyo.
Akiongea baada ya mazoezi ya jana, mshambuliaji Haji Ugando, alisema kuwa Coastal ni timu nzuri na ina mwalimu ambaye anajua ugumu wa ligi hivyo kama mchezaji anafuata maelekezo ya kocha huku yeye binafsi akijiandaa kuhakikisha anacheza mechi zote.
Kwa upande wake Moses Kitandu ambaye msimu uliopita alikuwa mshambuliaji chaguo la pili baada ya John Bocco kwa wekundu wa msimbazi, yeye amekiri kuwa mzunguko wa ligi ni mrefu lakini amejiandaa kushirikiana na wenzake ili kuipa timu hiyo matokeo mazuri.
Kwa upande wake kocha wa timu hiyo Juma Mgunda, ameeleza kuwa kila mchezaji anajituma na kuonesha uwezo kwenye mazoezi. ''Tunafanya mazoezi mara mbili kwa siku na wachezaji wananipa imani kuwa tutashindana kwenye ligi''.
Coastal United ni miongoni mwa timu 6 ambazo zimepanda ligi kuu msimu huu. Timu hiyo ilishuka daraja msimu wa 2016/17, ikacheza ligi daraja la kwanza msimu wa 2017/18 na kufanikiwa kurejea ligi kuu na itaanza msimu wa 2018/19, Agosti 22 kwa kuikaribisha Lipuli FC.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
