Monday, October 7, 2019

Sifa za wanawake wanaopendwa


Mara nyingi wanaume wengi hupenda wanawake wenye sifa zifuatazo katika mahusiano ya kimapenzi;

Wenye msimamo
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

Wapenda usawa
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

Wenye urafiki ndani yake
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.

Wanaojitegemea
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

Wanaoridhika
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

Thursday, October 3, 2019

Reuben Ndege "Nchakali" Kavae Viatu vya Jasiri RUGE uingoze njia Clouds FM

Nimepatwa na furaha sana baada ya kuona taarifa kwenye ukurasa wako wa mtandao wa Instagram ukiufahamisha umma/mashabiki kuwa kwa sasa umerejea CMG, Clouds Media Group, imekuwa furaha kwa wengi ila hofu kwa wengi pia.

Reuben Ndege almaarufu Nchakali, ulipikwa Clouds na jasiri marehemu Ruge ukawa zao bora na hatimae SCANAD wakaona hapana wakakukaribisha na kukupa nafasi uuoneshe uuma upande wako wa creativity uko vipi.

Ukiwa SCANAD ulipaza sauti na wachache hawakuelewa ila walioko kwenye tasnia ya Advertisement waliumia kichwa na kuwaza haya madini huyu mtu anayatoa wapi, Kampuni kubwa umeshiriki kuandaa kampeni za bidhaa kwa njia ya matangazo, Coca Cola, Vodacom, Tigo, Kvant, Chai Bora, etc.

Naweza sema uzalendo na Upendo ulionao Clouds ndio umekurejesha na ni heshima kwa Ruge huko aliko anatabasamu nakuona viatu vyake mvaaji amepatikana,sidhani kama umeangalia sana maslahi, kama ni maslah SCANAD naamin walikuwa na uwezo wa kukuretain kwa nafasi uliokuwa nayo na ungebaki ila la hasha.

Wengi walijiuliza viatu vya jasiri angevaa nani, na jina lako lilikuwa midomoni mwa kila mtu naona ule msemo wa Sauti ya watu ni sauti ya Mungu umejidhihirisha, kapambane na tukutakie kila kheri wale waliohisi Mawingu imefika Mwisho nadhani wameanza kuona ndio kwanza Imezaliwa upya.

Kila la heri Reuben Ndege (Nchakali).


By Mayowela

NCHIMBI,MOLINGA BALAA SANA....WAPIGA SHOO YA KIBABE YANGA IKITOKA SARE NA POLISI

Na  Olipa Assa - Mwanaspoti
 Mshambuliaji, Ditram Nchimbi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu kufunga hat trick msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania.

Nchimbi amefunga mabao hayo Leo Alhamisi wakati timu yake ya Polisi Tanzania ikilizimisha sare 3-3 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Nchimbi alifunga mabao yake katika dakika ya 34, 55 na 58 na kuifanya Yanga kuwa nyuma kwa mabao 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Hata hivyo furaha hiyo ya Polisi Tanzania ilidumu kwa muda mfupi baada ya mshambuliaji David Molinga akifunga mabao mawili katika dakika ya 65 na 68 kuisawazishia Yanga.

Hayo ni mabao ya kwanza kwa Molinga kufunga katika Ligi Kuu Bara, moja akifunga goli la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliipigwa na Ngassa kabla ya kupachika la pili kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kuamsha shangwe za mashabiki wa Yanga.


Molinga hakuanza vizuri dakika 45 za mwanzo alirejea kwa kishindo na kuwapa nguvu mashabiki wa Yanga waliokuwa nyuma kwa mabao 3-1 hadi dakika ya 64.

Lissu asaini mkataba na kampuni ya kimataifa kumsimamia kisheria


Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesaini mkataba maalum na kampuni ya kimataifa ya kisheria ya Amsterdam and Partners LLP akiwapa jukumu la kusimamia haki zake za kikatiba na za kimataifa.

Kampuni hiyo imetoa taarifa yake jana, Oktoba 2, 2019 ikieleza kuwa imefurahi kufanya kazi na Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

"Tunajivunia kufanya kazi na Tundu Lissu katika kuongeza uelewa kwenye hali yake na kampeni dhidi ya uvunjifu wa sheria na haki za kisiasa," imeeleza kampuni hiyo.

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji tangu Januari 6, 2018 alipoenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa kwa risasi, alitangaza kuahirisha kurejea nchini Septemba 7 mwaka huu kama alivyoahidi ili akutane kwa mara nyingine na madaktari wake.

Mwanasiasa huyo alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa maeneo ya nyumbani kwake, Area D jijini Dodoma.

Alipatiwa matibabu ya awali katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kisha akapelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi, kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji alikoendelea kupatiwa matibabu hadi leo.

Kampuni ya Amsterdam and Partners LLP yenye makazi yake jijini London nchini Uingereza, kazi yake kubwa ni kuwashauri wateja hususan kwenye changamoto kubwa za kisheria.

Wanawake Waonywa Kuhusu Kutumia Mvuke wa Moto Sehemu za Siri


Madaktari wa magonjwa ya wanawake wameonya kuhusu hatari inayotokana na kutumia mvuke wa moto kwenye sehemu za siri, baada ya kutokea kuwa mwanamke mmoja alijiunguza sehemu zake za siri alipo kuwa akitumia mvuke wa maji kufusha au kufukiza sehemu za siri.

Waswahili husema urembo unauma. Je ni maumivu kiasi gani unayoweza vumilia ili kupata urembo au kupendeza?
4h

MGANGA WA KIENYEJI ADAIWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 8 MAMA AKINUNUA WEMBE


Mganga wa kienyeji mkazi wa Ujiji, Venas Edward (48), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Mkoa wa Kigoma kwa madai ya kumbaka mtoto msichana mwenye umri wa miaka minane.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Katoki Mwakitalu, mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana.

Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Raymond Kimbe, ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Akisoma maelezo ya awali Wakili wa Serikali Kimbe, alidai kuwa Aprili 23, mwaka huu majira ya asubuhi eneo la Kasoko-Ujiji, mshtakiwa huyo alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka minane na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Kimbe alidai siku ya tukio mtoto huyo alichukuliwa na mama yake mzazi (jina linahifadhiwa) na kwenda naye kwa mshtakiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kwa ajili ya kupata matibabu.

Alidai baada ya kufika kwa mganga huyo mama wa mtoto aliambiwa aende kununua kiwembe dukani na kumuacha mtoto na mganga huyo, ambaye anadaiwa alitumia nafasi hiyo kumbaka mtoto huyo.

Kufuatia tukio hilo ilidaiwa mshtakiwa huyo alikamatwa na askari polisi na baada ya mahojiano alipelekwa mahakamani.

Wakili huyo alidai upande wa mashtaka unatarajia kupeleka mashahidi watano pamoja na kielelezo kimoja cha PF 3 na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi.

Hakimu Mwakitalu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 9 kwa kusikilizwa.

Source

Friday, September 27, 2019

Bashe Asema kuna upotevu wa zaidi ya Bilioni 120 kwenye vyama vya ushirika



Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi ya shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), wamebaini kuwepo kwa upotevu wa jumla ya shilingi Bilioni 123 kwenye vyama vya ushirika.

Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa bodi ya pamba nchini kinachofanyikia kwenye ukumbi wa benki kuu (BOT) jijini Mwanza ambapo ameeleza kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua kali.

"Hapa nina kabrasha, nitawapatia wakuu wa mikoa wote na nitamkabidhi kiongozi wa tume, kwa ripoti ya COASCO ushirika kumetokea jumla ya upotevu wa sh. Bilioni 123, na nisema hapa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika wote," amesema.

"Hizi ni pesa za wakulima, wote waliohusika katika huu upotevu watachukuliwa hatua kali na wakuu wa mikoa tutawapa majina ya Amcos gani wanahusika na mnatakiwa kuchukua hatua," amesema Bashe.

Aidha ameongeza kuwa ushirika uliopo kwa sasa unahitaji mabadiliko makubwa kwani hauwezi  kutatua matatizo ya kilimo hasa kwenye zao la pamba, ambapo mfumo unatakiwa kubadilishwa kutoka ushirika wa kuhudumia wakulima na kuwa ushirika wa kibiashara.

DC MWAIMU AWATANGAZIA KIAMA WANAOJUMU MIRADI YA MAENDELEO KYERWA

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mh. Rashid Mwaimu

Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Mhe. Rashid Mwaimu 
amesema atapambana vikali usiku na mchana ili kuhakikisha anakomesha watu wanaotaka kuhujumu miradi ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi itolewayo na serikali akibainisha kuwa yupo tayari kukesha katika maeneo yote ya miradi ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya hiyo Rashid Mwaimu ametoa kauli hiyo Septemba 27.2019 ofisini kwake wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo wilayani hapo.

Mhe.Rashid amesema atahakikisha analinda na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayoletwa na serikali wilayani humo huku akiahidi kuwashughulikilia wale wanaokutaka kufanya vitendo vya kuihujumu serikali.

Amesema kutokana na jitihada, nguvu na busara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika utekelezaji wa miradi ya ki maendeleo yeye kama mkuu wa wilaya hatomfumbia macho mtu yeyote anayepanga kuhujumu miradi hiyo.

"Nawaahidi miradi yote inayoletwa na serikali kwa ajili ya wilaya ya Kyerwa nitaisimamia na kuilinda kwa nguvu zote, nitahakikisha adui yeyote haisogelei miradi hiyo ,miradi ni mali ya wananchi ole wenu mliozoea kuitafuna muda umekwisha, nitacheza na nyie usiku kucha", alisema Mwaimu.

Hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuwahimiza kutomchagua kiongozi mbishi, badala yake wachague kiongozi ambaye ni mzalendo na muadilifu atakayewaletea maendeleo.

Katika suala la ulinzi na usalama, amesema katika wilaya yake ulinzi na usalama ni wa kutosha hivyo amewataka wananchi kuripoti katika vyombo husika mara moja vinapojitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani kwa baadhi ya watu wasiowaadilifu hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

KITABU CHA KUSAIDIA WANAWAKE WANAOWANIA NAFASI ZA UONGOZI CHAZINDULIWA KWENYE TAMASHA LA JINSIA 2019


Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukifanyika leo  Alhamis Septemba 26,2019 kwenye usiku wa Mwanamke wa Kiafrika wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. Lengo la kitabu hicho ni kutoa taarifa muhimu kuhusu mashirika yanayosaidia jitihada za wanawake kuwania nafasi za uongozi kwa ngazi zote na kwa wanawake wa vyama vyote vya siasa. Kitabu hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Women Fund Tanzania kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya na Seidel Foundation. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change' ukiendelea.
Wanawake wakifurahia wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change'.
Wanawake wakifurahia wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha 'Women Leaders Power of Change'.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...