Friday, July 12, 2019

MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2019 ATEMBEZEWA KICHAPO NA WAANDAAJI WA SHINDANO

Na Marco Maduhu na Kadama Malunde -Malunde1 blog.

Mshiriki wa mashindano ya ulimbwende mkoani Shinyanga (Miss Shinyanga 2019) Nicole Emmanuel, amedai kupigwa na kuvuliwa nguo hadharani na waandaji wa mashindano hayo wa Kampuni ya  Burudani ya Makumbusho Entertainment mjini Shinyanga wakati akidai fedha zake nauli shilingi 70,000/=.

Tukio hilo limetokea jana Julai 11,2019 majira ya saa 11 jioni kwenye hotel ya Nedman iliyopo ushirika Shinyanga mjini Miss huyo akiwa na mshiriki mwenzake wa shindano hilo aitwaye Agnes Masunga walipofika kwenye hoteli hiyo(kambi waliyokuwa wanaitumia) ili kudai nauli zao.

Waandaji wa Shindano hilo wanaotuhumiwa kumpiga na kumdhalilisha binti huyo ni Meneja Mkuu wa Makumbusho Entertainment,George Foda na Mkurugenzi wa Makumbusho Entertainment Richard Luhende ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika SHIRECU mkoa wa Shinyanga.


Akizungumza na waandishi wa habari Miss huyo Nicole, alisema wakati wakiwa kwenye ushiriki wa mashindano hayo ya Miss Shinyanga ambayo yalifanyika Julai 6 mwaka huu, waliahidiwa kuwa kuanzia mshindi wa nafasi ya 4 hadi 13 watapewa kifuta jasho cha Shilingi 50,000 pamoja na nauli ya kurudi kwao lakini kwake hali ikawa tofauti.

"Baada ya mashindano kuisha na mimi sikubahatika kushinda Taji hilo la U miss Shinyanga,sikuingia kwenye tano bora, ikabidi niombe fedha zangu za nauli jumla shilingi 70,000 ili nirudi Dar es salaam nilikokuwa lakini nikaanza kuzungushwa pamoja na SMS za kutakwa kimapenzi,"alisema mrembo huyo.

"Leo mimi na mwenzangu Agnes Masunga tulienda Nedman kufuata nauli zetu,nikamuomba Meneja George anipe pesa zangu akasema Mkurugenzi hajaafiki mimi kupewa nauli,nikamwambia basi mimi naenda polisi kudai haki yangu,nikatoka,nilipofika getini nikamwambia bodaboda awashe pikipiki tuondoke ndipo George na Luhende wakanifuata na kuanza kunipiga vibao,kunivua nguo 'kuchana nguo yangu ya ndani',kuniburuta chini,kunivuta nywele kunikaba shingo na kisha kunipeleka polisi wakidai nimefanya vurugu,"aliongeza.

"Wamenipeleka kituoni nikiwa uchi,'walichana nguo yangu ya ndani' kwenye gari alikuwemo Richard Luhende na George Foda wameenda kusingizia polisi kuwa mimi nimefanya vurugu wakati mimi nadai haki yangu,walikuwa wananitisha kuwa wao wana hela na madaraka watanifanyia kitu kibaya sitakaa nisahau katika maisha yangu..wamenipiga wameniumiza jicho la kushoto,mguuni nina jeraha,bega linauma baada ya kuruburutwa chini,kichwa kinauma kwa kuvutwa nywele",alieleza.

"Nilivyofika kituoni Luhende akasema niwekwe ndani na kwamba atawapigia simu polisi baadae,akaja askari kunisikiliza baadaye akaja Mkuu wa kituo cha polisi ndiyo akawa amenisaidia pale,akawa anawauliza kwanini wamenifanya vile,nikamhadithia na mimi kile kilichotokea,ikaishia pale ndipo Luhende akanipa Shilingi 100,000 ili niondoke kituoni,lakini hakunipa gharama zozote za matibabu",alifafanua Mrembo huyo.

Kwa upande wake,Mwendesha bodaboda Japhet Kazimili aliyeshuhudia tukio la mrembo huyo kupigwa alisema akiwa getini alishuhudia Nicole akipigwa mtama na kuchaniwa nguo kisha kuwekwa ndani ya gari na George na Luhende huku dada huyo akilia akiomba msaada.

Hata hivyo meneja mkuu Makumbusho Entertainment George Foda, licha ya kudai waandishi wa habari wamekurupuka,alikanusha kumtembezea kichapo Miss huyo huku akikiri kwamba ni kweli mrembo huyo alikuwa anawadai pesa na katika kudai pesa hizo alianza kuleta fujo hotelini ndipo wakamchukua na kumpeleka kituo cha polisi.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) Richard Abwao, alikiri binti huyo kufikishwa Polisi na kubainisha kuwa ameshapewa pesa yake aliyokuwa anaidai na kama binti huyo atafungua kesi polisi watampa ushirikiano.

Aidha Mama mlezi wa binti huyo Grace Elias ambaye pia ni mama mzazi wa Agnes Masunga ambaye naye alikuwa akidai fedha yake, alilaani kitendo hicho cha waandaji wamashindano hayo ya Miss Shinyanga kuwafanyia ukatili wa kijisia watoto hao kwa kuwadhalilisha kingono pamoja na kuwapiga pale wanapodai haki zao.

Grace Elias alisema binti yake amekaa kambini siku 15 na akiwa kambini alipoteza simu yake ya shilingi 270,000/= lakini waandaji wa shindano hilo hawakutoa ushirikiano ili simu ipatikane lakini pia binti yake pia hakuingia kwenye tano naye hakupewa kifuta jasho chake na baada ya kusumbuana nao sana ndiyo amepewa shilingi 50,000/- baada ya kufikishana polisi.

Kampuni ya Makumbusho Entertainment pia ni Waandaaji wa Shindano la Miss Lake Zone linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni Mkoani Shinyanga. 

VIDEO: Hatutaki urasimu katika uwekezaji - RC Mwanri


Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akiwa katika kikao cha kujadili na kutengeneza mkakati wa kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuendana na kasi ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USIKOSE KU-SUBSCRIBE...

RAO HEALTH TRAINING CENTRE RORYA YATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

MKUU WA CHUO CHA RAO HEALTH TRAINING CENTRE RORYA ANATANGAZA KUPOKEA MAOMBI KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020 KWA INTAKE YA SEPTEMBER.

 KATIKA KOZI ZIFUATAZO:

 1. ORDINARY DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (AFISA TABIBU) MIAKA 3 SIFA ZA MWOMBAJI:

AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA ANGALAU ALAMA 'D' IKIWEMO FIZIKIA'D' BIOLOJIA'D' KEMIA'D' NA IKIWEMO HESABU NA ENGLISH NI KWA NYONGEZA KWA MASOMO MOJAWAPO.

 2. CETIFICATE IN IN CLINICAL MEDICIN (AFISATABUBU MSAIDIZI) MIAKA MIWILI

SIFA ZA MWOMBAJI:
AWE NA UFAULU WA KIDATO CHA NNE KWA MASOMO ANGALAU ALAMA 'D' IKIWEMO MASOMO YA FIZIKIA'D' BIOLOJIA 'D' CHEMIA'D' NA IKIWEMO HESABU NA KINGEREZA KWA MASOMO MOJAWAPO


FOMU ZINAPATIKANA CHUONI RAO MKOA WA MARA WILAYA YA RORYA AU KWENYE WEB SITE YETU www.raocoop.org 

au wasiliana nasi kwa Email raohtc@raocoop.org au 0753624780 / 0758084663 / 0757862200 / 0763358409 / 0785191131/ 0784383329

WAHI SASA NAFASI NI CHACHE!!!!!! ALL COREESPONDENCES BE ADDRESS TO THE DIRECTOR GENERAL












Vanessa Mdee responds after she was accused of snatching Elizabeth Micheal’s husband!


Vanessa Mdee has brushed off rumors linking her to Majizzo who happens to be engaged to Lulu Micheal.

This is after she was spotted on several occasions in the company of the fella thus sparking rumors that they were secretly involved.

However, turns out that Vanessa and Majizzo are just good friends and business partners since they happen to be in the same line of business.

Speaking during a live session with her Instagram family, Vanessa opened up saying;

"Kabisa yule ni kakangu ni mtu na mheshimu tunafanya biashara pamoja ni mtu ambaye ni mdau wa music and we love that girl we love Lulu and that's her husband. What are you all talking about?!"

Juma Juxx new girlfriend
When asked about her exes new girlfriend, Ms Mdee revealed that she had no idea who the lady was nor did it bother her.

Vanessa Mdee went on to add that they have been apart for 9 months now and just like everyone else, she found out about her exe's new lady via Instagram.

Juzi kati Juma amemtambulisha mpenzi wake mpya nyinyi kupitia Instagram na mimi tumefind out the same time. Juma na mimi tumeachana tuna miezi Zaidi ya tisa. Tumeachana in a way ya kwamba tulijua tukifanya public itaaffect watu wengi, isitoshe sisi tuna vitu vingi ambavyo tunafanya kwa pamoja kibiashara. Kuna vitu vingi ambavyo tunamiliki pamoja in terms of joint interests. Kuna vitu ambavyo tulikuwa tumepanga kufanya kwa pamoja and that was the reason hatukuwa na pupa kutangaza kuachana kwetu mapema.

Thursday, July 11, 2019

TFF yamtangaza atakaye kinoa kikosi cha Taifa Stars

Kikao cha Kamati ya dharura cha Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambacho kimekutana leo,kimemtangaza Kocha Mkuu wa Azam Ndayiragije Etienne  kuwa Kaimu Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.


VIDEO: Majmbazi 7 wanaswa Dar, gari linalohuisika na ulifu lawekwa chini ya ulinzi


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za wizi wa bajaji maeneo ya Ukonga.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao walivunja maduka matatu na kufanikiwa kuiba bidhaa mbalimbali, fedha pamoja na bajaji mbili zenye namba za usajili MC 312 CFB aina ya TVS na MC 540 CED aina ya TVS zote zikiwa na rangi ya bluu.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE  

Wednesday, July 10, 2019

Vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kuvitumia

Vipo vitu mbalimbali ambavyo mama mjamzito hapaswi kuvitumia wakati wa ujauzito kwani vina athari kubwa sana kwake yeye mwenyewe pamoja na mwanaye aliye tumboni.

Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na;

1. Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto hivyo hairuhusiwi kabisa kutumia kwa kipindi hicho.

2. Uvutaji Sigara.

3. Unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.

4. Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.


Hospital mpya ya rufaa Njombe yaanza kutoa huduma




Na Amiri kilagalila-Njombe

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amefungua zoezi la utoaji wa huduma ya afya katika hospital mpya ya rufaa ya mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alipokuwa na ziara ya siku tatu kuanzia april 9 mwaka huu mkoani humo.

Akizungumza na wananchi kabla ya kukabidhi hospital hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka amesema kuwa awali mkoa wa Njombe ulikuwa ukitumia hospital ya kibena iliyochini ya halmashauri ya mji wa Njombe kuwa hospital teule ya mkoa.

Ili kuendelea kuboresha na kusogeza karibu huduma za afya mkoani humo waziri Ummy amesema kuwa hospital ya kibena haitoweza kuondolewa kifaa chochote huku akitoa wito kwa halmashauri ya mji wa Njombe kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa katika hospital hiyo.

"Hamkufanya makosa halmashauri kutukabidhi hospital ile ya kibena ninyi wenyewe ni mashahidi baada ya kuwa imeteuliwa hospital teule ya mkoa,hali ya utoaji huduma ilibadirika,sasa niseme pale katika hospital hatutaondoa.

chochote,na mimi ni matumaini yangu kwamba halmashauri mtaendelea kuboresha ili ipatikane huduma bora".

Katika hatua nyingine waziri Ummy amemkabidhi site mkandarasi  ili kuanza ujenzi wa majengo 7 ya kisasa katika ujenzi wa hatua ya pili na kumpa mkandarasi miezi 8 mpaka 10 na kumpongeza Rais kwa kutoa bilioni 7.65 kwa ajili ya ujenzi huo.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka mara baada ya kuishukuru serikali kwa kuzindua huduma katika hospital hiyo,ameagiza halmashauri kuweka utaratibu mzuri wa usafiri ili wananchi waweze kupata huduma kufika katika hospital hiyo.

Mganga mfawidhi wa iliyokuwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Njombe kibena Dkt.Winferd Kiambile,amesema miongoni mwa huduma zitakazotolewa katika hospital mpya ni pamoja na kliniki za kibingwa.

"Mh waziri nikuhakikishie kwamba watoa huduma tupo tayari kutoa huduma katika hospital hii,huduma zitakazotolewa ni  huduma za OP zote vile vile kuna kliniki za kibingwa,na huduma nyingine nyingi"

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo wamesema kuwa kuanza kutumika kwa hospital hiyo kutawapunguzia gharama kwa kuwa awali walikuwa wakifuata huduma kubwa za rufaa katika mikoa jirani ikiwemo Mbeya na Iringa.

Hospital ya rufaa ya mkoa wa Njombe kwa wagonjwa wa nje, awamu ya kwanza ya ujenzi umegharimu bilioni 3.2

SANAMU YA MWALIMU NYERERE BURIGI- CHATO YAZUA GUMZO MTANDAONI

Jana Julai 9, 2019 kulikuwa na hafla ya uzinduzi wa Hifadhi mpya ya wanyamapori ya Burigi-Chato, Hafla ambayo ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumkabidhi Sanamu hiyo ya Baba wa Taifa. 

Rais Dkt. Magufuli alitoa maelekezo kuwa Sanamu hiyo aliyokabidhiwa ijengewe eneo zuri katika hifadhi hiyo ya Burigi Chato ili watalii wakija waweze kumjua zaidi Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli alikabidhiwa sanamu ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla yenye ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyama pori.

Muonekano wa sanamu hiyo, umezua mijadala tofauti tofauti kwenye mitandao ya kijamii wengi wakionekana kushangazwa na muonekano wake wakidai kuwa hauendani hata kidogo na sura ya Mwalimu Nyerere.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...