Monday, March 1, 2021

Serikali yaondoa zuio la kula kitimoto mikoa ya kanda ya Ziwa


Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeondoa marufuku ya uuzaji na ulaji wa nyama ya Nguruwe katika Wilaya sita za Kanda ya Ziwa ambazo zilikumbwa na Homa ya Nguruwe (ASF) mwezi mmoja uliopita

Prof Hezron Nonga, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, amesema ASF imeondoka katika Wilaya hizo lakini Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera bado haijatangazwa kuwa salama, na hivyo marufuku inaendelea

Wilaya nyingine ambazo zilitangazwa kuathirika ni Mbogwe na Geita katika Mkoa wa Geita, Sengerema na Missungwi katika Mkoa wa Mwanza, Kyerwa katika Mkoa wa Kagera na Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.


Ahsanteni Tanzania kwa ukarimu wenu – Mamelodi Sundowns




Maimba ya soka nchini Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns Football Club wamewashukuru Watanzania kwa ukarimu wao katika kipindi walichokuwa hapa nchini wakijiandaa na mchezo wao wa klabu bingwa Afrika.



Mamelodi wamefanikiwa kuwafunga CR Belouizdad magoli 5 – 1 ambao ndiyo waliyokuwa wenyeji baada ya Waalgeria hao kuuomba Uongozi wa Shirikisho la Mpira nchini Tanzania TFF kuutumia uwanja wa Mkapa kama dimba lao la nyumbani hapo jana.

"Tunaondoka na magoli matano na pointi 3 lakini mioyo yetu inabakia Tanzania! 🇹🇿. Ahsanteni sana kwa ukarimu wenu!," wameandika Mamelodi Sundowns.

Magoli ya Sundowns yalifungwa na (5′, 55′ Zwane, 48′ Shalulile, 75′ Maboe, 89′ Erasmus) wakati lile la wenyeji CR Belouizdad likifungwa na (44′ Sayoud).

Rais Mwinyi ateua mrithi wa Maalim Seif



RAIS wa Zanzibar, Hussein Mwinyi, amemteua Othuman Masoud Othuman wa ACT-Wazalendo kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani humo, kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad, aliyefariki dunia 17 Februari 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 1 Machi 2021 na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Zena Said imesema, Othuman ataapishwa kesho Jumanne, Ikulu visiwani humo.

Othuman, anachukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad (77), aliyefariki dunia tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif, alifikwa na mauti wakati akiendelea na matibabu hospitalini hapo tangu 9 Februari, alipofikishwa akitokea Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Zanzibar.


 
Othuman, amewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Zanzibar.


Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar
Mara baada ya Dk. Ali Mohamed Shein, kuingia madarakani mwaka 2010, alimteua Othuman kuwa mwanasheria mkuu wa serikali Novemba 2010; nafasi aliyohudumu hadi Oktoba mwaka 2014, uteuzi wako ulipotenguliwa.

Othuman alikumbana na dhahama hiyo, kutokana na misimamo yake, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Zanzibar, kwenye mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.


Othuman, alikuwa muumini wa serikali tatu na kupigania kupunguza mambo ya muungano na kupiga kura ya wazi ya kupinga mambo kadhaa yahusiyo Zanzibar, jambo lilikuwa tofauti na msimamo wa CCM.

Kutokana na msimamo huo, Othuman alitimliwa ndani ya Bunge Maalum la Katiba, jijini Dodoma na kurejeshwa Zanzibar, ambako nako, alikutana na rungu la Dk. Shein la kumvua wadhifa huo.


Maalim Seif Sharrif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Othuman ambaye ni mzaliwa wa Pandani, Pemba, mbali na shughuli zake za kisheria anazozifanya ndani na nje ya Zanzibar, aliendelea kusimamia msimamo wake wa haki ya Wazanzibar akiamini kwenye serikali tatu, kama ilivyokuwa kwa Maalim Seif.

Ni miongoni mwa wanachama wenye kupanga mikakati ya ndani ya ACT-Wazalendo ya kuweza kuibuka mshindi na kwa kipindi chote, amekuwa karibu na viongozi wakuu wa chama hicho.


 
Othuman alianza kuwa karibu na Maalim Seif, katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2020, na alikuwa miongoni mwa timu maalum iliyoandaa ilani ya uchaguzi huo kupitia ACT-Wazalendo.


 


MBUNGE ANENGUA KIUNO LIVE MBELE YA WANANCHI AKICHEZA NGOMA YA DIAMOND PLATNUMZ


Mbunge Aisha Jumwa aliwatumbuiza wananchi wakati wa kampeni za UDA eneo la Matungu baada ya kunengua kiuno akicheza wimbo maarufu wa Diamond, Waah 
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa aliwanengulia wakazi wa Matungu kiuno.
**
Mbunge wa Malindi nchini Kenya Aisha Jumwa amewachangamsha wakazi wa Matungu baada ya kunengua kiuno chake akicheza wimbo wa Diamond Platnumz wa Waah wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo ujao.

Jumwa alikuwa anampigia debe mgombea wa United Democratic Alliance (UDA) Alex Lanya ambapo alimuomba DJ kumchezea wimbo wa Diamond wa Waah ili kuwathibitishia wakazi ana kipaji cha kutingisha kiuno.

Punde wimbo huo maarufu ulipopasua anga, mwanasiasa huyo mashuhuri alianza kutingisha kiuno chake na kuwafurahisha wakazi.

Huku akiwa amezamishwa na muziki, baadhi ya wakazi walijiunga pamoja naye kwenye jukwaa na kumsaidia kuwatumbuiza wenzao ambao walishindwa kuficha furaha yao Jumwa akisakata ngoma.

 Uchaguzi Mdogo wa Machi 4,202.

Katika hotuba yake, mwanasiasa huyo wa Tanga Tanga aliwaomba wakazi kumpigia kura mgombea wa UDA, Lanya katika uchaguzi mdogo wa Machi 4 ambapo atamenyana na wagombea wengine 15. 

Alisema viongozi wa Magharibi kama vile Musalia Mudavadi na Francis Atwoli wamekuwa wakiwapoteza wakazi wa eneo hilo kwa muda mrefu.

 "Siku hiyo ya uchaguzi, ninawaomba nyinyi nyote mumpigie kura Lanya ili tuweze kurejea tena kuanza safari ya kuingia Ikulu pamoja," alisema.

Kama ilivyoripotiwa awali, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iliwaidhinisha wagombea 15 kuwania kiti hicho ambacho kilisalia kufuatia kifo cha Justus Murunga. Wagombea hao ni ikiwemo Bernard Wakoli, Gregory Atoko, Kevin Nectus, Wilberforce Lutta, Athman Wangara, Anzelimo Kongoti na Samuel Munyekenye. Wengine ni Peter Nabulindo (ANC), David Were (ODM), Alex Lanya (UDA), Charles Kasamani (UDP), Paul Achayo (MDG) na Faida Auma wa Maendeleo Chap Chap.

Chanzo - Tuko News

Wanne wafariki kwa ajali wakitokea kwenye mapumziko


Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Watu wanne akiwemo mkuu wa chuo cha uuguzi Lugarawa Steven Mtega (39) wamefariki dunia kwa kuzama kwenye mto Lupali wakiwa kwenye gari waliyokua wakisafiria kata lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Akizungumza kwa njia ya simu jana mganga mkuu  wa wilaya ya Ludewa dkt Stanley Mlay,alisema tukio hilo limetokea febuari 27 majira ya usiku marehemu hao walikua kwenye gari aina ya harrier ambapo walikua Lugarawa kwenye mambo yao ya mapumziko.

"Walipata ajali kwenye mto lupali huu mto sasa hivi una maji mengi kwa sababu ya mvua zinavyonyesha walikua watu wanne kwenye mambo yao ya mapumziko Lugarawa na dereva alikua huyo mkuu wa chuo wakasema wabadilishe maeneo waende Mundindi sasa walivyofika maeneo hayo ndo wanaingia mtoni" alisema Mlay.

Mlay aliwataja marehemu wengine kuwa Marko Mpete,fundi umeme wa Lugarawa

Merk Mwalongo(35)mjasiriamali

Rukia Mfaume(28) alikuwa mhasibu wa mradi wa umeme wa Akra Lugarawa

Hata hivyo alisema miili ya marehemu hao iko chumba cha kuhifadhia maiti(Mochwari)Hospital ya Lugarawa ikisubiri taratibu za mazishi kukamilishwa.

Naye diwani wa kata ya Lugarawa Erasto Mhagama,akizungumza kutokea kwa tukio hilo alisema tukio hilo limetokea mpakani kwa kijiji cha shaurimoyo na kijiji cha amani.

Biden kutoa tamko kuhusu Saudi Arabia leo


Rais wa Marekani Joe Biden amesema leo Jumatatu, Machi 1, Serikali yake itatoa tamko juu ya Saudi Arabia kufuatia ripoti ya kijasusi ya Marekani kusema kuwa mrithi wa kiti cha Ufalme wa taifa hilo, Mohammed Bin Salman aliamuru mauaji ya muandishi habari Jamal Khashoggi.

Utawala wa Biden umekosolewa hasa katika ripoti ya gazeti la Washington Post iliyosema Biden angeonesha nguvu zake kwa Salman ambaye hakuwekewa vikwazo vya aina yoyote licha ya kutajwa kuhusika na mauaji ya Khashoggi.

Biden amesema atatangaza leo Jumatatu hatua watakayochukua kwa Saudi Arabia.

Jamal Khashoggi aliyekuwa uhamishoni Marekani akiandika ripoti zinazomkosoa, Mohammed Salman na Serikali ya Saudi Arabia, aliuwawa Oktoba 2, 2018, katika Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki.

Wanaswa na vipande 13 vya meno ya tembo wakisaka wateja





Kikosi maalum ya kupambana na ujangili katika eneo la ikolojia ya Tarangire – Manyara, kimewakamata watu wawili katika  kijiji cha Moyaka wilaya ya Babati mkoani Manyara wakiuza vipande 13 vya meno ya tembo.


Mkuu wa kikosi cha kuzuiwa ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini, Peter Mbanjoko leo Februari 28 amethiitisha kukamatwa watuhumiwa hao, Benard Masalu na  Yembeson Masumbuko na kupongeza kazi nzuri ambayo imefanywa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Burunge WMA na Chemchem ambao wamewekeza katika eneo hilo.



"Nimepata taarifa za tukio hili na tayari watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea," amesema.



Mtendaji mkuu wa Taasisi Chemchem Assosiation, Walter Pallangayo amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na taarifa za siri ambazo walizipata na wakaandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwao.



Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza hoteli za kitalii na kufanya utalii wa picha katika eneo la Burunge WMA imekuwa na mfuko maalum wa kupambana na ujangili ambapo kwa mwaka Sh400 milioni zinatumika  kufanya operesheni katika eneo hilo la ikolojia ya  Tarangire – Manyara.

Kocha Simba Aiwekea Mtego Yanga




WAKATI mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara zikiwa bado mbili, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema licha ya kushiriki mashindano mengi tofauti, lakini hawajasahau michezo yao mitatu ya viporo kwenye ligi hiyo ambayo wanataka kushinda ili kuishusha Yanga kileleni.

 

Hivi sasa Simba inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imekusanya pointi 42 baada ya kucheza mechi 18, ikizidiwa pointi saba na vinara wa ligi hiyo, Yanga wenye pointi 49 zilizotokana na kucheza mechi 21 ambazo ni tatu zaidi ya Simba.



Kesho Jumatatu, Simba inatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na JKT Tanzania katika mchezo wa kiporo wa ligi kuu, utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Endapo Simba ikifanikiwa kushinda mechi zate tatu za viporo, basi itaishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na kukaa mabingwa hao watetezi kwa tofauti ya pointi mbili.

 

Akizungumza na Spoti Xtra,Gomes alisema: "Hivi karibuni ratiba yetu imetubana kidogo kwani tumekuwa na michezo mingi ya michuano tofauti, lakini ni jambo zuri kuona tunapata matokeo mazuri kwenye michezo yote.



"Licha ya michuano mingi tuliyonayo, lakini nikuhakikishie bado tunakumbuka kuwa tuna michezo mitatu ya ligi ambayo lazima tushinde, kwani tunataka kushika usukani wa ligi katika kipindi hiki ambapo ligi inaelekea ukingoni ili kujihak-ikishia malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu."


Epuka tabia hizi kama kweli unataka kufanikiwa

 

Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.

Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi nikiwa na maana ya kwamba binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye kikombe na umgorogee  na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi,  kitu cha kujiuliza je mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu. 

Mtu huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema sifanyi biashara yeyote ile mi nipo tu, ukimuuliza kwanini haufanyi biashara yeyote  tatizo nini? Utamsikia anakujibu tatizo mtaji huku akiamini kuwa mataji pekee katika biashara ni fedha. Ndugu msomaji wa makala hii hata uwe na fedha kiasi gani kama huna wazo kwa ajili ya matumizi ya fedha, hata ukipewa milioni mia moja leo  hizo pesa zitaisha utajikuta mwisho wa siku huna hata mia mbovu. Watu wengi tunatazama mitaji kama fedha peke yake ukitazama katika msingi huo utazidi kulamu mpaka mwisho huku maisha yakiendelea kuwa magaumu.

 Ngoja nikuibie siri mtaji unaweza ukaupata kwa kutumia ujuzi pamoja nguvu ulizonazo ili kutengeneza bidhaa au huduma zitazokufanya upate fedha.  Kwa mfano Wewe mwenye elimu juu tekinologia ya habari na mawasiliano unaweza ukabili ujuzi wako kuwa bidhaa kwa kuwa fundi wa computer na kutengeza progamu mbalimbali. Swali la kujiuliza unaweza vipi kubadili ujuzi ulio nao kuwa bidhaa au huduma hapo ndipo wengi tunapofeli kwa sababu ni wavivu wa kufikiri.

Naendelea kumchambua binadamu ili uone ni jinsi gani tulivokuwa na tabia za lawama. Binadamu huyo huyo utamkuta  anaishi mazingira machafu ambayo yatasababisha muda wowote magonjwa ya mlipuko kutokea, ukimfuta bianadamu huyo na kumuuliza unafikiri ni kwanini  mazingira haya ni machafu, utamsikia jibu atakalokupa atakwambia tatizo ni serikali, binadamu huyohuyo utamkuta hana ajira ila ukimuuliza kwanini  hauna ajira? Atakujibu tatizo ni serikali.

Kuna msanini mmoja wa hip-hop anaitwa nikki mbishi aliwahi imba kwenye wimbo huku akiuliza serikali ni nini? Maana imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila kitu. Ndugu msomaji wa makala haya nakusihi na kukushauri pia kwa kile ambacho unaweza kukifanya usisubiri serikali ndio ukifanyie, kama unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako fanya usisubiri kuambiwa, maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa wanasubiri kuambiwa fanya hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya mafanikio kwa upande wako yatakuja kwa asilimia chache sana.

Kitu cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na msingi wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata Yule unayemlalamikia hakusikii na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu kwa moyo mmoja bila kusubiri mtu Fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke usemi huu "kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari''

Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini upo hapo ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa Kiswahili unasema kila binadamu ni mchunga ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma makala hii endapo utaulizwa Swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha uone una thamani gani mbele ya watu wengine?

Na: Benson Chonya
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...