Tuesday, January 7, 2020

Mfanyabiashara Kutoka India Yuko Nchini Kuangalia Fursa Za Uwekezaji

Mfanyabiashara kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku saba kuanzia tarehe 6 hadi 12 Januari 2020. Bw. Agwarala ambaye amekuja kuangalia fursa za uwekezaji nchini, atafanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya CRDB, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na kutembelea maeneo kadhaa kwa lengo la kupata maelezo kuhusu taratibu na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Maeneo yatakayotembelewa na mfanyabiashara huyo ni Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) Dar es Salaam, Mkoa wa Simiyu ambapo ataangalia uwezekano wa kupata eneo la ekari elfu mbili (2,000) kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha mpunga na ujenzi wa kiwanda zao hilo. Bw. Agarwala atatembelea maghala ya pamba ili kujiridhisha kabla ya kununua kiasi cha robota laki moja (100,000) ambayo aliahidi kununua wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya CRDB mwezi Desemba 2019.

Bw. Agarwala pia atatembelea machimbo ya Tanzanite, mkoani Manyara, Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi kilichopo mkoani Iringa na kuangalia uzalishaji maparachichi ili kujenga kiwanda cha kusindika zao hilo kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi.

Ujio wa mfanyabiashara huyo ni matokeo ya juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini India ambao uliratibu ziara ya kikazi iliyofanywa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts iliyofanyika nchini India mwezi Desemba mwaka jana. Ziara hiyo ililenga kutafuta wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la pamba nchini humo.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.



Source

BASATA YAMFUTIA USAJILI MSANII DUDUBAYA ...SASA MARUFUKU KUJIHUSISHA NA SANAA


Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini, Dudubaya amefutiwa usajili na baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ambapo  baraza hilo pia limetoa onyo kwa taasisi, kampuni na mtu yeyote kutofanya kazi na msanii huyo. Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kukataa wito wa baraza hilo.





Dudubaya ambaye jina lake halisi ni Godfrey Tumaini alitakiwa kufika ofisi za Basata leo Januari 7, 2020 saa 4:00 asubuhi baada ya kusambaa kwa video zake kwenye mitandao ya kijamii akizungumzia mambo mbalimbali, ambapo Basata imeeleza ametumia kauli zisizokuwa na maadili wala staha.


Hata hivyo, Dudubaya aliukataa wito huo kwa kulijibu baraza hilo kuhangaikia kwanza na migogoro iliyopo kati ya baadhi ya vyombo vya habari na wasanii ili kuufanya muziki usonge mbele huku maneno aliyoyatumia katika video zake akieleza kuwa ni ya kawaida.

Kutokana na kutoitikia wito huo, Katibu Mtendaji, wa baraza hilo, Godfrey Mngereza katika tamko lake hilo amesema baraza limechukua hatua ya kumfutia usajili wake kuanzia leo Januari 7,2020.



Meddie Kagere Afunguka Kuhusu HIRIZI Aliyovuliwa Uwanjani 'Ni Cheni Yangu ya Dhahabu Siyo Hirizi Jamani"




HUKO mitani na hata kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wa Yanga wamemzulia kitu straika wa Simba, Meddie Kagere baada ya sakata lake na beki Kelvin Yondani, lakini mwenyewe amewasikia na kuwaambia "acheni hizo, ile ni cheni yangu ya dhahabu tu".

Katika pambano la juzi lililoisha kwa sare ya 2-2, Ally Mtoni 'Sonso' aliyekuwa anakabana na Kagere aliiona cheni shingoni mwa straika huyo na kumtonya Yondani ambaye aliikata kijanja kabla ya kukimbilia kwa mwamuzi Jonesia Rukyaa kulalamikia kuvaa kwake cheni hiyo.

Hata hivyo, kulitokea purukushani kidogo na mashabiki kuzua eti ili 'busta', lakini Kagere amesema hana mambo hayo ya kipuuzi na kwamba ile ni cheni ya dhahabu na alipitiwa tu kuivua kabla ya kuingia uwanjani, lakini imechukuliwa sivyo ndivyo.

Alisema alikuwa amevaa cheni hiyo kabla ya mchezo kuanza na hata alipokwenda kupasha misuli alikuwa nayo na alijisahau kuivua walipoenda vyumba vya kubadilishia nguo, alisahau kuvua na akaingia nayo uwanjani.

"Nilijikuta nimeingia nayo uwanjani na kuanza kucheza, lakini wakati Yondani ananikaba aliivuta na kuikata, huku akienda kumueleza mwamuzi nacheza nikiwa na cheni jambo ambalo aliichukua na kuipeleka katika benchi letu," alisema na kuongeza:

"Huwa naivaa muda mwingi kwani hata nikiwa nimelala nakuwa nayo, ndio maana nilijisahau kuivua na nilijikuta nipo nayo uwanjani na muda ambao nilijua kuwa ninayo ni ule Yondani alivyoikata, lakini hakuna kingine cha ziada na mlipoona natafuta kitu ni kidani cha herufi K."

Naye beki wa kulia wa Simba, Shomary Kapombe aliyeshuhudia sakata hilo alisema hakuona kitu chochote tofauti na cheni ya Kagere ambayo Yondani akiwa katika harakati zake za kumkaba aliivuta na kuikata.

"Ni cheni yake ya dhahabu iliyokatwa na Yondani na pale tulipokuwa tunashangaa ilikuwa tunatafuta kidani chenye herufi ya jina lake, lakini tulishindwa kukipata kwa vile mechi ilikuwa ikiendelea," alisema Kapombe.

Source

VIDEO: Mapya kesi ya Tito Magoti na mwenzake, taarifa ya upelelezi yaelezwa mahakamani


Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili ofisa wa Programu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania, Tito Magoti (26) na mtaalamu wa Tehama, Theodory Giyama (36) wameuomba upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wa kesi kwa wakati ili haki iweze kutendeka

Magoti na Giyani wanakabiliwa na makosa matatu likiwamo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh 17 milioni, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam hata hivyo hawana dhamana kutokana na shtaka la utakatishaji fedha linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Saturday, January 4, 2020

VIDEO: Mkwasa ailipua Simba, tuligundua madhaifu yao ''tumecheza na timu inayoongoza kupewa penati''


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amefunguka kuhusiana na mchezo wao dhidi Simba ambapo uliomalizika jioni hii ambapo amesema wametumia madhaifu ya wapinzani wao na ndio maana kipindi cha pili wamefanya vizuri

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI........USISAHAU KUSUBSCRIBE


Source

Mwanahabari wa DW Adaiwa Kulishwa Sumu



Deokaji Makomba ambaye ni Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa Hospitalini hapo akiwa hajitambui.

Alikutwa akiwa amepoteza fahamu ndani ya basi la Ally's. Imeelezwa kuwa alikuwa umelala usingizi mzito na ikabainika kuwa ameibiwa mizigo yake.

Mwandishi huyo alitoka Jijini Mwanza kwa basi hilo na ameeleza kuwa alipewa vipande vya Biskuti na abiria aliyepandia njiani na ndipo akapoteza fahamu.

Mwanahabari huyo licha ya kueleza kuwa anaendelea vizuri lakini amekiri kuwa hana nguvu na bado anahitaji kulala zaidi ili kupumzisha mwili wake.

Mwanaume unapaswa kukumbuka hili katika mahusiano yako

Mwanaume acha ubahiri kwa sababu ni maagizo ya Mungu mwenyewe. In fact ni furaha ya mwanamke yeyote yule kuwa na mwanaume anaeweza kumhudumia mahitaji yake licha ya mwanamke nae kujikwamua kiuchumi kama ziada na nyongeza tu lakini sio wajibu wake.

Mwanaume Mungu anapokubariki na kipato sio vibaya ukamfanyia vitu vizuri mwanamke wako anataka manicure au pedicure.

Mpe fedha akaweke mwili katika mwonekano bomba! Mfanyie hata suprise ya shopping mara moja moja. Tuache ubahili, tusihonge pembeni tutafilisika, vichenchede vya nje huwa vinakamua mpaka unabaki na sharubu tu! tujifunze kuwahonga wake zetu!

Anataka vacation, peleka Ngorongoro huko huyo baby wako akashangae tembo. Anataka kula vitu vizuri, give her the treat. Kazi yako kama mwanaume ni kuhakikisha mwanamke wako anaridhika na anafurahia uwepo wako.

Kila mwanamke ni mzuri, inategemeana na wewe utakavyompa kipaumbele!

Mwanamke nae asibweteke, Mumewe anaporudi nyumbani huku akiwa na furaha ya kufanikisha dili kadhaa au huzuni ya kufeli kwa dili zake ampe mumewe maneno matamu ya kutia moyo pamoja na vitu adimu kitandani afurahie uwepo wako.

Thursday, January 2, 2020

Upande wa Jamhuri wakataa Kabendera kumzika Mama yake...Mahakama Kuamua

Upande wa Serikali umempa pole Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi huku ukipinga maombi yake ya kutaka ashiriki Ibada ya mazishi ya mama yake.

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Kabendera anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha alipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.

"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba,"amesema Wankyo.

Wankyo amedai kuwa maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia Mkurugenzi wa Mashitaka hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

"Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini mahakama isifungwe mikono," amesema.

Kuhusu mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefika hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP).

Kukataliwa kwa Kabendera kushiriki mazishi ya Mama yake, kumeibuka kutokana na maombi aliyoyatoa Kabendera kupitia Mawakili wake akiwemo Jebra Kambole.

Wakili Kambole amedai wanaiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Changombe majira ya mchana.

Kambole ameieleza mahakama kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha.

"Kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake tutakuwa tumemuadhibu adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza na ni vizuri akatoa heshima ya mwisho,"ameeleza.

Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.

"Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho," ameomba.

Baada ya kutoa hoja hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.


Wednesday, January 1, 2020

Mahakama ya Angola imeagiza mali za mtoto wa rais zikamatwe



MAHAKAMA ya Angola imeagiza kukamatwa kwa mali na akaunti za benki za bilionea ambaye ni binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Bi Isabel Dos Santos.

Kukamatwa kwa mali hizo kunatokana na mipango ya serikali iliyopo kukabiliana na ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Utawala wa Rais Joao Lourenco unataka kuchukua takriban dola bilioni moja ambazo umekuwa ukimdai Bi Isabel Dos Santos na washirika wake.

Amepinga madai hayo na kusema kwamba hajafanya makosa yoyote wakati babake alipokuwa mamlakani.

Akidaiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, Bi Dos Santos anakadiriwa na jarida la Forbes kuwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 2.2.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 anaishi ughaibuni, akisema kwamba aliondoka Angola kwa kuwa maisha yake yalitishiwa.

Anaendesha biashara kubwa akiwa na kampuni nchini Angola na Portugal ambapo anamiliki hisa katika kampuni ya Nos SGPS.

Mahakama iliagiza mali ya Bi Santos kupigwa kuchukuliwa ikiwemo akaunti zake za benki mbali na hisa zake katika kampuni nchini Angola, ikiwemo ile ya Unitel na Benki ya Fomento de Angola (BFA) kilisema chombo kimoja cha habari cha serikali ambapo naye alisema anashutumu kile alichokitaja kuwa shambulio linaloshinikizwa kisiasa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...