Tuesday, August 26, 2025

DOTTO BAHEMU AMEWAOMBA WANA - CCM KUVUNJA MAKUNDI NA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KUTAFUTA USHINDI WA KISHINDO

 

Dotto Bahemu baada ya kukabidhiwa na msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara 
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara Bwana Constatino Msemwa ( aliyeko upande  wa Kulia )  akimkabidhi Fomu Dotto Bahemu fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Ngara kupitia chama cha Mapinduzi 
Dotto Bahemu akisaini kwenye kitabu cha Wageni baada ya kufika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara


Na Mariam Kagenda _Kagera

Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara kupitia Chama cha Mapinduzi Dotto Bahemu amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuvunja makundi na kuungana kwa Pamoja ili kukiwezesha   chama hicho kupata ushindi wa Kishindo  kwa Rais, Mbunge na Madiwani 

Bahemu amesema hayo leo Agosti 26,2025  baada ya kuchukua fomu ya Uteuzi wa kugombea Ubunge Jimbo la Ngara katika ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara .

''Uchaguzi wa kura za maoni umeisha na kila mmoja alikuwa na kundi lake hivyo sasa  ni jukumu letu sote kuungana kwa pamoja kutafuta kura za kishindo kwa Rais wetu, Mbunge na madiwani wote wanaotokana na chama cha mapinduzi",amesema Dotto Bahemu.

Ameongeza kuwa atashirikiana na kila mtu hata ambao walikuwa hawamuungi mkono wakati wa uchaguzi wa kura za maoni   na kati ya watu atakaoanza kuwatafuta na kuzungumza nao  ni wale ambao walikuwa hawamuungi mkono  na hawakuwa upande wake ili kujua tatizo liko wap  huku akiwaomba wananchi wa Jimbo la Ngara kudumisha amani katika kipindi chote cha Uchaguzi.

Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ngara Constantino Msemwa amesema kuwa Dotto Bahemu amekabidhiwa fomu hiyo baada ya kutimiza  Vigezo na masharti yote.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Bwana Ndaisaba Ruholo amesema atampatia ushirikiano wa Kutosha Dotto Bahemu katika kipindi chote cha Uchaguzi na kuwaomba wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi Jimbo la Ngara kumpa ushirikiano Mgombea aliyeteuliwa na CCM.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...