Saturday, May 3, 2025

MADIWANI KISHAPU WAPEWA NASAHA KIPINDI CHA LALA SALAMA



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shija Ntelezu akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani la kujadili taarifa za kamati za kudumu robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025

Na Sumai Salum- Kishapu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga  Shija Ntelezu amewakumbusha madiwani  kipindi hiki cha mwisho kwenda kukamilisha miradi mbalimbali iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi Kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo amesema hivi karibuni kwenye mkutano  wa baraza la madiwani la robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025 la kujadili taarifa za kamati za kudumu huku akisisitiza ukamilishaji vyumba vya madalasa Busangwa, Ndoleleji,mwamala na maeneo mengine.

Ni kweli tuko kipindi cha kumalizia endeleeni kufanya kazi kama mlivyokuwa mkifanya uwepo wa maboma ya muda mrefu unatia aibu, nia yangu mkawaambie wananchi kama wanatakiwa kumalizia wachange wamalizie na kama ni serikali basi mwenyekiti mnapomalizia miezi hii mhakikishe maboma yote yanakamilika" amesema Ntelezu

Ntelezu amesema kwa karne iliyopo wananchi wanahitaji sana  maendeleo si Chama pekee hivyo wanapaswa kuhakikisha nguvu za wananchi hazipotei bure kwa maboma waliyoanzisha kutokamilishwa ili wapate huduma waliyoitazamia.

Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi amesema serikali inaendelea kusogeza mahitaji yote muhimu kwa wananchi wa maeneo yote na Kishapu imekuwa miongoni mwa Wilaya bora inazosimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ubora na wakati.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema madiwani bado wanaowajibu wa kuelimisha jamii zao kuhusu ulipaji kodi kwani serikali inategemea faini,ushuru na kodi ili kuleta maendeleo.
 
"Mhe.Mwenyekiti hakika umekuwa kiongozi wa mfano kuongoza Halmashauri kwa umoja na mshikamano bila vurugu lakini pia madiwani mmempa ushirikiano mkubwa yeye na Mkurugenzi wetu katika kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi niwapongeze sana" ameongeza Masindi

Amesema madiwani hao wamekuwa kwenye baraza hilo kwa kuwasilisha ipasavyo sauti za wananchi wanaowaongoza na wamepaza sauti zao katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu,afya,maji,barabara na umeme na serikali imetekeleza kwa kiwango kikubwa na bado itaendelea kufanya ikiwemo ujenzi wa kiwango cha rami barabara ya Kolandoto Mhunze.















Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...