
Na Lydia Lugakila - Kagera
Faris ametoa pongezi hizo katika kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Kyerwa mkoani kagera katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo ikiwa ni ziara ya siku 16 kutoa elimu ya uraia juu ya kupiga kura kutafuta wapiga kura wapya vijana.
Amewapongeza wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa walioketi Machi 10 mwaka huu kwa kupitisha kauli mbiu mpya ambayo itatumika 2025 -2030 ikiwa ni kauli mbiu mpya ambayo italeta maendeleo makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujmla hivyo vijana wanapaswa kuiishi na kuiweka katika mioyo yao.
Kupitia vikao mikutano mkusanyiko wa kampeni ya siku 16 mkoani Kagera elimu ya uraia kwa vijana wa CCM inaendelea kutolewa kuhakikisha wanashiriki uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika mwaka huu.
"Tunatoa elimu ya uraia kwa vijana hatubagui vijana wa rika zote ambao wamefikisha umri wa kujiandikisha kuhakisha wanajiandikisha na kupiga kura mwaka huu kwa sababu utamaduni wa vijana wengi hawapigi kura wanaongelea vijiweni ,tunaamini hii kampeini italeta mabadiliko makubwa kwa vijana sambamba na kuwaasa vijana kuchukua fomu za kugombea udiwani na ubunge ili waweze kutimiza ndoto zao," amesema.