Sunday, August 8, 2021

WATU 105,745 TAYARI WAMEPATA CHANJO YA CORONA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata chanjo ya UVIKO-19 Julai 28,2021 ikiwa ni sehemu ya uzinduzi ili ianze kutumiwa na Watanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona wimbi la Tatu.

Na Veronica Mrema

Watu 164,500 wamejiandikisha kupata chanjo ya CORONA na kati yao 105,745 tayari wamepata chanjo hiyo, kulingana na tathmini iliyotolewa leo Jumapili Agosti 8,2021 na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Tathmini hiyo inaeleza idadi hiyo ya watu ni ndani ya siku 11, ikihesabiwa tangu Julai 28, mwaka huu hadi kufikia Agosti 7, mwaka huu ilipozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu ndogo ya Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Abel Makubi amesema idadi hiyo ya watu ni katika makundi ya walengwa waliotajwa katika kipaumbele.

" Serikali inachukua hii nafasi kuwapongeza sana wananchi na viongozi walengwa kwa mwitikio mkubwa wa kuchanja," amesema.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...