Monday, July 12, 2021

Wafanyabishara watatu Dar Wadakwa na Dawa za Kulevya





Wafanyabishara watatu wa jijini Dar es Salaa wakiwa chini ya jeshi la Polisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

 

Wafanyabishara watatu wa jijini Dar es Salaa wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 1.02.

 

Wakili wa serikali , Yusuph Aboud akisoma hati ya mashtaka amesema washtakiwa hao kuwa ni  Andrew Paul (34) Mkazi wa Kurasini, Said Mugoha (45) Mkazi wa Mtoni Kijichi Temeke na George Mwakang'ata (38) Mkazi wa Mbagala Kuu.

 

Washtakiwa hao wamesomewa Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo ambapo imedaiwa Juni 21,2021 huko Mivinjeni ndani ya Wilaya ya Temeke Dar es Salaam, walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 1.2 huku wakijua ni kinyume cha sheria.

 

Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu.

 

Upande wa mashtaka umedai upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 27 mwaka huu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...