Na Rahel Nyabali, Kigoma.
Dawati la jinsia chini limetakiwa kuondoa dhamana kwa watuhumiwa wamakosa ya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji hatua ambayo itasaidia ukomeshwaji wa matukio hayo.
Ameyasemahayo Naibu waziri wa Wizara ya afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Mwanaidi Hamisi Katikaziara mkoani Kigoma alipotembelea Dawati la jinsia la wilaya ya Kigoma baaadaya kupokea ripoti ya miezi sita ya matukio ya ukatili ambapo kati ya kesi 128 kesi 6 Pekee watuhumiwa wamehukumiwa Vifungo.
Mratibu wa Dawati la JinsiaWilayaya Kigoma Mary Boniphas amesema ushirikiano mdogo wa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia unasababisha kushindwa kufikia hukumu kwa wakati au kufutwakabisa kwa kesi hizo.
"Changamoto kubwa inayo tukabili ikifika wakati wa kutoa ushahidi familia nzima na wahanga hawapatikani mwisho wasiku kesi inafutwa kwa kukosa ushahidi" amesema Mary Boniphas Mratibu wa Dawati la JinsiaWilayaya Kigoma.
Baada ya kupata maelezo hayo Naibu waziri Mwanaidi kwanza akazitaka idara zote zinazo shughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia kuondoa urasimu katika uendeshaji wakesi hizo ili kuharakisha utoaji wa haki kwa Wahanga
"Jambo hili litapungua endapo washukiwa wa matukio haya watanyimwa dhamana tusioneane haya tukifanya hivyo matukio haya yatapungua"amesema Mwanaidi Hamisi. Naibu waziri wa Wizara ya afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto.
Adha amewaagiza maafisa ustawi wa jamii kuwapatia vitambulisho wazee wote wenyeumri unaostahili ili waweze kupata huduma za afya bila malipo katikaVituo vya afya kote nchini.