Sunday, July 18, 2021

Maandamano yaibuka kupinga sheria ya Corona Ufaransa


Zaidi ya watu laki moja wameandamana kote Ufaransa kupinga hatua za hivi karibuni za serikali za kuwashinikiza watu kwenda kuchanjwa.



Serikali inalenga kuzuia maambukizi ya virusi vipya aina ya Delta vinavyo sambaa haraka.



Huko Paris, maandamano tofauti ya mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto yalitawala sehemu tofauti za jiji kuanzia Strasbourg mashariki, Lille kaskazini, Montpellier kusini na kwingineko.



Maelfu ya watu waliitikia wito wa kuandamana kutoka kwa mwanasiasa wa mrengo wa kulia Florian Philippot, mpambe wa zamani wa Marine Le Pen ambaye alitangaza mapema mwezi huu kwamba atawania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Philippot aliandaa maandamano madogo na ya kawaida dhidi ya serikali katika kushughulikia janga la corona lakini maandamano hayo yalivutia umati mkubwa zaidi na kwa upana walioathirika na siasa za taifa hilo.

Waandamanaji walilaani uamuzi wa serikali uliotolewa siku ya Jumatatu kufanya chanjo ya lazima kwa wafanyikazi wote wa huduma za afya, na kuhitajika kwa hati ya kuthibitisha huna maambukizi au umechanjwa kikamilifu ili kufikia mikahawa na maeneo mengine ya umma.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...