Sunday, July 18, 2021

Bei ya ufata yaongezeka, wakulima wahimizwa kuwahi msimu


Na Ahmad Mmow, Nachingwea. 

Bei ya ufuta katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi imeongezeka  katika mnada wa sita kwa chama hicho  uliofanyika leo. 

Mnada huo uliofanyika katika kijiji cha Kiangara, wilaya Liwale bei ya juu ni shilingi 2,593. na bei ya chini ni shilingi 2,556 kwa kila kilo moja. 

Kwamujibu wa kaimu mrajisi msaidizi wa ushirika wa mkoa wa Lindi, Richard Zengo jumla ya tani 1,706 na kilo 130 zimenunliwa kwenye mnada huo ambao ni  wa 14 kwa mkoa wa Lindi kwa msimu wa 2021. Kwani chama kikuu cha Lindi Mwambao kimeshafanya minada nane. 

Zengo alisema ufuta huo upo katika maghala makuu manne yaliyopo katika wilaya za Liwale, Ruangwa na Nachingwea. 

'' Ghala la Umoja lina tani 674 na kilo 32, Ghala la Lipande lina tani tani 471 na kilo 25, Zuma tani 389 na kilo 61 na Shamsi tani 172 na kilo 12. 

Kwahiyo mzigo ulionunuliwa leo ni tani zote 1,706 na kilo 130,'' alisema Zengo. 

Zengo alibainisha kwamba katika ghala la Umoja(Liwale) bei ya juu ni shilingi 2,560 na bei ya chini shilingi 2,556, ghala la Lipande(Ruangwa) bei ya juu shilingi 2,593 na bei ya chini shilingi 2,290 na maghala ya Shamsi na Export(Nachingwea) bei ya juu shilingi 2,593 na bei ya chini ni shilingi 2,53. 

Kaimu mwenyekiti wa RUNALI, Shemsia Naruchonga alitoa wito kwa wakulima ambao hawajapeleka ufuta wao sokoni wapeleke ili kuwahi bei na msimu. 

Kwani matarajio nikufunga msimu tarehe 25.07. 2021 au 30.07.2021 iwapo makusanyo yatendelea kuwa makubwa. 

Naruchonga pia alisema msimu huu hakuna changamoto ya kuchelewa malipo ya wakulima, vifungashio, ufuta mchafu na hata tatizo la wakulima kuchanganya taarifa zao limepungua. 

Katika mnada wa tano uliofanyika mjini Ruangwa tarehe 11.07.2021 ambao zilinunliwa kilo 452,182, bei ya juu ilikuwa shilingi 2,577 na bei ya chini shilingi 2,574. 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...