Tuesday, July 20, 2021

Hii Ndio Aina ya Silaha Iliyotumika na Muuaji Aliyemuua Mwenzake na Kujiua Mwenyewe



Miongoni mwa matukio ya kutisha wikiendi iliyopita ni lile la mfanyabishara Alex Korosso almaarufu Simba kumuua mwenzake, Gift na yeye mwenyewe kujiua baada ya kutokea mabishano kati yao.

Tukio hilo lilijiri Jumamosi iliyoita katika Baa ya Lemax iliyopo Sinza-Kwa Remmy jijini Dar.


Sasa, mjadala mikubwa umekuwa ni aina ya silaha iliyotumika, lakini kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya silaha wanasema silaha ile ni bastola (pistol) ndogo (short-gun) aina ya revolver.


Wanasema hii ni silaha ya moto inayoshikwa kwa mkono mmoja tu. Teknolojia yake ni karibu sawa na ya bunduki isipokuwa yenyewe ni ndogo.


Kiasili bastola hii ina umbo dogo na kila baada ya mapigo kadhaa huhitaji kujazwa upya na ina chemba ya risasi inayozunguka ndiyo maana huitwa revolver kutokana na mzunguko wa chemba.



Ni rahisi kujaza chemba ya ziada na kuibeba kama akiba inayobadilishwa haraka kuliko kujaza upya chemba inayozunguka kwa sababu chemba ya kuzunguka haitolewi.


Faida yake ni kuwa nyepesi na ndogo, hivyo haisumbui mtu wakati wa kubeba.

Jeshini bastola hii hutumiwa kama silaha ya pili pamoja na bunduki. Kwa Polisi huwa ni silaha kali ya kawaida. Majambazi mara nyingi hupendelea kuitumia kwa sababu inafichwa maungoni kirahisi na haionekani.


Hiyo ndiyo silaha inayodhaniwa ilitumika kwa maana ya watu walioiona kwa macho, lakini Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kupitia kamanda wake, ACP Ramadhani Kingaio linasema kuwa, linafanya uchunguzi kuhusu uhalali wa umiliki wa silaha iliyotumika kwenye tukio la vifo vya wawili hao.

Stori na Sifael Paul
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...