Saturday, June 26, 2021

Waajiriwa wapya 9,675 wa ualimu, afya hawa hapa

Dodoma. Serikali ya Tanzania imetangaza watumishi wapya 9,675 wa kada za elimu na afya walioajiriwa kufuatia kibali cha ajira kilichotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, Aprili, 2021.

Majina ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika tovuti ya ofisi ya Rais-Tamisemi ya www.tamisemi.go.tz.

Watumishi hao wapya wametangazwa na katibu mkuu ofisi ya rais Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe.

ORODHA YA WATUMISHI WA AJIRA MPYA KADA ZA AFYA

Profesa Shemdoe ametangaza ajira za  elimu 6,749 kwa shule za msingi na sekondari na wataalamu wa afya 2,726.

Amesema waombaji wa kada ya ualimu walikuwa 99,583  na wataalam 37,437 wa kada ya afya wakiwe

"Baada ya kukamilisha taratibu zote za uchakataji wa maombi walimu 6,949 (3,949 wa shule za msingi na 3,000 wa shule za sekondari) na wataalam wa kada za afya 2,726 wamepangiwa vituo vya kazi," amesema Profesa Shemdoe

Amewataka waajiriwa wapya kuripoti kwa wakurugenzi na kufanya kazi kwenye vituo walivyopangiwa na sio katika makao makuu ya halmashauri.

ORODHA YA WALIMU WA AJIRA MPYA

Profesa Shemdoe amewataka waajiriwa wapya kuripoti katika vituo vyao vya kazi wakiwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na sita, vyeti halisi vya kitaaluma vya kuhitimu mafunzo katika kada husika, kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho ya Nida pamoja na cheti halisi cha kuzaliwa.

Pia, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri ambazo zimepangiwa waajiriwa wapya kuwapokea na  kuwawezesha   kwa   kuzingatia  sheria, kanuni,  taratibu   na miongozo  ya utumishi wa umma na  baadaye kutoa  taarifa ya kuripoti kwao katika ofisi ya rais Tamisemi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...