Thursday, June 24, 2021

UEFA yafuta sheria ya bao la ugenini katika mashindano ya vilabu

 


Sheria ya bao la ugenini imefutwa na shirikisho la Kandanda Ulaya - UEFA baada ya miaka 56 kama njia muhimu ya kuamua mshindi wa mechi katika mashindano yake ya vilabu. 

Hatua hiyo aghalabu ilipendekezwa katika miaka ya karibuni na makocha wa vilabu ambao walihisi kuwa wazo hilo la miaka ya 1960 halikuwa na maana tena. 

Mechi ambazo sasa matokeo yake ya jumla yatakuwa ni sare baada ya dakika 90 za mkondo wa pili, zitaenda moja kwa moja katika muda wa ziada na kisha kuamuliwa na mikwaju ya penalti. 

Rais wa UEFA Alexander Ceferin ametaja "ukosefu wa haki, hasa katika muda wa ziada, wa kuihitaji timu ya nyumbani kufunga mara mbili wakati timu ya ugenini imefunga." 

UEFA imetanja sababu kadhaa zilizoamua suala hilo la mechi ya nyumbani na ugenini, ikiwemo matangazo zaidi ya televisheni, kuelewa zaidi mbinu za mchezo wa wapinzani, kusafiri vizuri na viwanja vizuri vya kucheza. 

Ceferin amesema sheria hiyo imepitwa na wakati na inazizuia timu za nyumbani dhidi ya kushambulia, kwa sababu zinahofia kufungwa bao ambalo litawapa wapinzano wao faida muhimu.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...