Simba, Al Ahly zikiwa zimeshafuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu huu.
Timu za Al Ahly na Simba leo zitakutana katika mchezo wa mwisho wa kundi A utakaochezwa katika Uwanja wa Al-Salam jijini Cairo, Misri kuanzia saa 4.00 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki.
Timu hizo zote mbili tayari zimeshajihakikishia tiketi ya robo fainali baada ya kushika nafasi mbili za juu.
Simba ikiongoza ikiwa na pointi 13 huku Al Ahly wakishika nafasi ya pili kwenye kundi hilo wakiwa na pointi 8.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo, AS Vita Club itaikaribisha Al Merrikh huko Kinshasa, DR Congo katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa De Martyrs katika muda sawa na ule wa mechi baina ya Al Ahly na Simba.