Monday, April 12, 2021

MWANAUME AJIUA BAADA YA KUKATALIWA NA MPENZI WAKE

Kijana aitwaye Kitachana Shenani (30) mkazi wa kitongoji cha Senta kijiji cha Makundusi Wilaya ya Serengeti mkoani Mara amejinyonga kwa kamba hadi kufa baada ya kukataliwa na mpenzi wake Pilly Kikono (39). 

Inaelezwa kuwa Pilly ambaye ni mfanyabiashara ya viatu katika kijiji cha Natta alimkataa na mpenzi wake Shenani mbele ya familia yake kwa madai kuwa amekuwa akimfanyia fujo akisema hamtaki atafute mwanamke mwingine hivyo achukue na asiende tena nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Makundusi Mseti Nyaikobe amesema walipata taarifa ya kujinyonga kwa kijana huyo kupitia wachunga mifugo siku hiyo ya tukio Aprili 11 majira ya saa 11 jioni.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...