Monday, April 12, 2021

Johnson and Johnson kusambaza chanjo EU

 


Nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) zimeanza kupokea chanjo ya Johnson and Johnson kutoka Marekani (USA) inayotolewa kwa dozi moja dhidi ya corona (Covid-19).


Msemaji wa Tume ya EU Stefan de Keersmaecker, alisema,


"Kulingana na makubaliano, dozi za kwanza ya chanjo ya Johnson and Johnson sasa ziko njiani kutoka kwa maghala kwenda nchi wanachama wa Jumuiya."


Chanjo ya Covid-19, ambayo inayotolewa kwa dozi moja iliyozalishwa na kampuni ya Johnson and Johnson, imekuwa ikitumika nchini Marekani pekee. Idhini inayohitajika kwa matumizi ya chanjo hiyo katika nchi za EU ilitolewa mnamo Machi 11.


Johnson and Johnson inatarajiwa kutoa dozi milioni 55 za chanjo kwa nchi za EU katika robo ya pili ya mwaka.


EU inapanga kufanya chanjo kwa asilimia 70 ya idadi ya watu wazima kupitia chanjo hizo za Covid-19 zitakazogawanywa kwa nchi wanachama mwishoni mwa Juni.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...