Spika wa Bunge, Job Ndugai amedai kuna upotoshaji mkubwa kuhusu mradi wa bandari ya Bagamoyo. "Tunaposisitiza utekelezaji wa mradi huu hatuna maana mbaya, hakuna mwenye mpango wa kuuza nchi hapa."
"Meli kubwa za kisasa ni karibu viwanja vitatu vya mpira, ni zaidi ya mita 300. Hakuna meli ya urefu huo inayoweza kuingia Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuwa mlango wake ni mwembamba na ni mdogo."