Israel inadaiwa kukumbwa na tatizo la uwasilishwaji wa chanjo dhidi ya corona (Covid-19).
Kulingana na taarifa za gazeti la Jarusalem Post, kampuni ya dawa ya Pfizer kutoka Marekani imesitisha kusafirisha chanjo kwenda nchini Israel.
Ilielezwa kuwa Israel bado haijalipia dozi milioni 2 za mwisho za chanjo walizoagiza. Usafirishaji wa dozi 700,000 za chanjo, ambazo zinatarajiwa kupelekwa nchini humo siku ya Jumapili, ulilazimika kucheleweshwa.
Redio ya Jeshi iliripoti kuwa maafisa wa Pfizer wanaichukulia Israel kama "jamhuri iliyokosa msimamo."
Hakukuwa na taarifa yoyote iliyotolewa na mamlaka ya Israel juu ya suala hili.
Taarifa zaidi zinadai kwamba tatizo la uwasilishwaji wa chanjo na malipo linahusishwa na mvutano wa kuunda serikali mpya nchini humo.