Wednesday, April 7, 2021

DIWANI AFARIKI DUNIA GESTI AKIWA NA MCHEPUKO


Diwani Kata ya Mbagala Kuu, Shabani Othman Abubakari enzi za uhai wake.

Na Dotto Mwaibale - Dar es salaam

DIWANI wa Kata ya Mbagala Kuu Shabani Othman Abubakari (CCM) amefariki dunia katika moja ya nyumba ya kulala wageni iliyopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam alipokuwa na mwanamke anayedaiwa ni mchepuko wake.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtimika na kuwa mazishi yake yatafanyika leo katika makaburi ya Tanita yaliyopo eneo la Kibonde Maji.

Mmoja wa wahudumu nyumba hiyo ya kulala wageni (jina lake linahifadhiwa) alisema diwani huyo alifika akiwa na gari lake wakiwa na msichana huyo usiku wa kuamkia juzi na kuchukua moja ya chumba katika nyumba hiyo.

Alisema asubuhi baada ya kuamka wakati akifanya usafi ndipo alipoukuta ufunguo wa chumba alichokuwa amekichukua diwani huyo na msichana huyo ukiwa umetupwa chini ambapo alishituka na kwenda katika chumba hicho na kukuta kikiwa kimefungwa na kilipofunguliwa walimkuta diwani huyo akiwa amefariki lakini yule msichana waliyekuwa naye hayupo.

Mhudumu huyo alisema baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi ambao walifika na baada ya kuwahoji waliuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...