Friday, March 5, 2021

Yanga mbovu, isingechukua ubingwa hatakama Simba haipo -Oscar Oscar na Geoffrey Lea




Maneno ya wachambuzi wa soka nchini Oscar Oscar na Geoflea baada ya Mwananchi, Yanga kupokea dhahama ya kipigo mbele ya Wagosi wa Kaya vijana wa Coastal Union hapo jana uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.



Oscar amesema Yanga walikuwa wanajificha kwenye kichaka cha kutofungwa, lakini ukweli ni kwamba wana mapungufu mengi. Oscar anasema kama Ligi yetu ingekuwa 'fair' kabisa kwamba mwenye kiwango kizuri anashinda, kama sio ukubwa na ukongwe wa Yanga, baasi Yanga hii isingeweza kuchukua ubingwa mbele ya timu nyingine hata kama @simbasctanzania isingekuwepo.

@geoff_lea ameunga na Oscar na kusema Yanga hawana timu nzuri. Ametoa mifano ya mechi kama mechi dhidi ya Gwambina, Polisi na nyingine ambazo Yanga walifaidikia na maamuzi mabaya ya marefa na kusema kwamba kama ligi ingekuwa 'fair enough' (usawa na haki ya kutosha) baasi Yanga wangekuwa nafasi ya 6 au ya 7 muda huu.

Ukiachia mbali kile kilichosemwa na wachambuzi hao mahiri nchini, Yanga inaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na jumla ya pointi 49 ikiwa imecheza michezo 22, nafasi ya pili ikichukuliwa na Simba SC wenye alama 45 wamecheza michezo 19, nafasi ya tatu Azam FC pointi 40 michezo 22.

IMEANDIKWA NA Hamza Fumo, Instagram @fumo255

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...