Nilikutana na rafiki yangu Frank jijini Dar baada ya kua tumepoteana tangia tulipomaliza sekondari O Level na kila mmoja wetu akapangiwa mkoa tofauti kwa masomo ya A Level. Sasa hivi yeye ni muajiriwa wa taasisi moja nyeti ya fedha na huku akiwa na biashara zake kadhaa
Tukawa na kawaida ya kuonana tunapopata nafasi na alipokua anakujua mitaa ninayokaa siku moja macho yake ya kaangukia kwa dada mmoja anaitwa Victoria. Kwa mwanaume uliyekamilika mara ya kwanza unapomuona Vicky huwezi kumuanagalia kwa mara moja lazima utamuangalia tena na tena! Itoshe kukwamambia Vicky alikua mzuri hasaa
Nilifanya juhudi hafifu(minimum efforts) kumzuia Frank asianzishe mahusiano na Vicky maana namjua Vicky nae akinijua japo tulikua hatujazoeana na sababu kubwa ni kwamaba mambo ya kumkataza mtu asiingea kwenye mahusiano yalishawahi kunitokea puani na kuna uzi nilileta humu
Mahusiano yao yalikolea haswaa na kwa muda mfupi Vicky akahamishwa na kupangishiwa nyumba sehemu nyingine, kukawa na safari za Nairobi, Bankok na Dubai ambapo alinunuliwa ka Vitz ili imsaidie kum shuttle mjini. Kiwanja cha nyumba nilikitafuta mimi baada ya kuombwa na Frank na bibie akawa anajengewa nyumba ambayo japo ilikua ndogo tu lakini ilikua nzuri na ikawa inapauliwa huku maandalizi ya finishing yanafanyika
Ikapita miezi kadhaa siku hiyo majira ya saa tatu asubuhi Frank ananipigia simu akitaka tuonane. Tulipoonana alikua mkimya na mtulivu na hakuweza kunywa hata breakfast aliyoagiza, kisha akatoa simu yake akanionyesha kitu amabacho kwakweli nikajifanyisha kushangaa lakini kwa ndani hata sikushangaa maana nilikitarajia kutokea siku moja, na baada ya hapo akanieleza kilichotokea
Yeye alikua ameoa na hakua na kawaida ya kulala nje ya kwake, na hata siku moja hakuwahi kupitisha usiku mzima nyumbani kwa Vicky. Hua anakaa tu hata ikiwa saa sita usiku anarudi kwa mkewe. Siku huyo mkewe alikua kasafiri akataka am surprise Vicky. Alipotoka kazini jioni alipitia kwa Vicky na ilipofika saa mbili usiku akaondoka. Na akiondoka hua harudi tena. Lakini siku hiyo ilipofika saa tano usiku akarudi tena nyumbani kwa sweetie wake asimkute
Kupiga simu mwanamke akawa kama yupo usingizini au ana fake kalala na akawa anasema yupo nyumbani na jamaa wala hakumshtua. Alikua na funguo zaake za nyumba hiyo akaingia ndani akakaa. Akawa anampigia kila baada ya nusu saa wanongea kawaida tu mwanamke anasema anatamani jamaa angekuwepo walale wote kwani amemmiss! Jamaa akalala hapo hadi asubuhi bila Vicky!
Kama Mungu tu, alipokua anaondoka asubuhi akawa amepaki gari yake opposite na ile nyumba anayokaa Vicky. ile Vitz ikawa inakuja inaendeshwa na mwanaume, Vicky yuko pembeni. Hawakujua kama kuna mtu na gari ile gari iliyopaki pembeni ya nyumba ya Vicky na wala hakuijua maana ni ya mke wa Frank. Ile Vitz haikua tinted sasa waliposimama tu wakaanza kunyonyana ulimi! Frank akapata ujasiri, mahali alipokua akaweza kuwapiga picha ya video kwenye simu na waliposhuka kufungua geti walikua wamekumbatiana na akaipata picha vizuuri!
Alichofanya Frank kesho yake akampigia simu Vicky aende akaangalie gari RAV4 kwenye yard flani ya kuuzia magari ya jamaa yake ili amnunulie aachane na ka Vitz(Nilikuja gundua Frank ndie mmiliki wa nyuma ya pazia wa yard hii) Alipofika akaambiwa ile RAV inauzwa 16mil na ishalipiwa na Frank 12mil kwa hiyo Vicky alipowasiliana na Frank akaambiwa kama amependa ni vizuri kwa hiyo atafute mteja faster wa vitz hata kwa milionne ili apate RAV ambayo Frank kashailipia 12 kwa akjili ya yeyeVicky! Kwa msaada wa madalali ndani ya muda mfupi akawa kashaiuza gari yake na akamtaarifu Frank
Frank akamwambia wala asisumbuke kulipa zile hela pale yard. kuna hela yeye Frank atapata kesho yake na watalipia gari. Akamwambia ajiandae wanasafari ya Nairobi kuna nyumba kali sana waliwahi kuiona huko sasa wakachukue ramani yake aje amjengee hiyo nyumba ya ramani watakayoifuata Nairobi aachane na kale kanyumba kadogo
Kwahiyo katika milioni nne alizouzia gari achukue milioni moja afanye shoping ya vyakula na nguo, milioni mbili aende kwenye kampuni flani ya ujenzi wakafanye demolition ya "kile kinyumba" alichokua anamjengea ili kutoa nafasi kwa nyumba ya ramani kali! Vicky ndio alichokifanya. Yaani ndani ya masaa nane katika siku moja akawa kauza gari na kabomoa nyumba kwa mshangao wa wengi mpaka mafundi walokua site, tena kabomoa yeye mwenyewe bila uwepo wa Frank around
Zoezi lote la uuzaji gari na ubomoaji nyumba lilipokamilika Frank akamtumia zile picha alizokua amenionyesha mimi na meseji ya kwamba kuanzia siku hiyo asahau kama aliwahi kua na mpenzi anaitwa Frank, wala hakutaka suluhu ya aina yoyote!
Kama Vicky angekua anapajua nyumbani kwa Frank angemfuata bahati (sijui nzuri au mbaya) alikua hapajui. Alikwenda kwenye ile yard ya magari akaambiwa Frank kaja kuchukua hela zake gari halitaki tena! Alijaribu kumfuata mara kadhaa ofiini kwake lakini bahati nzuri taratibu za kuingia pale ni ngumu. Alikuja kwangu na akaniachia kizaazaa na wife kua nimetokana nae wapi maana anajulikana mambo yake! Kwa ufupi alichanganyikiwa akapagawa yule binti aisee
Ni muda mrefu toka yatokee hayo na jana nimekutana na Victoria. Yeye ndie alienikumbuka. Mimi ningemsahau! Amebadilika, amechoka, amezeeka! Sijui nini kimesibu shemeji yangu. Nilimpatia hela kidogo ya soda akashukuru sana na nikachukua namba yake baade niliongea na Frank(Yupo Mwanza sikuhizi) akanambia nimpe hiyo namba atamtumia chochote kimsaidie kidogo. Sija check nae kujua kama alishafanya hivyo
By Sesten Zakazaka
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...