Tuesday, March 16, 2021

GEKUL AITAKA TALIRI KUJIENDESHA KIBIASHARA


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Viongozi wa NARCO na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kongwa wakati alipotembelea Ranchi ya Kongwa kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi wilayani humo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na wachungaji wa ng'ombe (waliosimama kushoto) wanaomilikiwa na taasisi ya TALIRI Mpwapwa wakati alipotembelea taasisi ya TALIRI na LITA Mpwapwa kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika. Waliosimama kulia ni Viongozi kutoka Wizarani, TALIRI, LITA na Viongozi wa Wilaya ya Mpwapwa.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Viongozi na watumishi wa TALIRI na LITA Mwapwapwa pamoja na viongozi wa Wilaya wakati alipotembelea taasisi hizo kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Mama Salma Kikwete (wa kwanza kulia) katika duka la nyama kwenye Ranchi ya Kongwa wakati alipotembelea Ranchi hiyo kukagua shughuli zinazofanyika.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Bw. Mnyonaki (wa kwanza kushoto) ambaye ni mfugaji na mkulima wa malisho ya Mifugo katika kijiji cha Msunjilile Wilayani Kongwa wakati alipomtembelea kwa lengo la kuona shamba lake la malisho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul (wa pili kutoka kushoto) akiangalia eneo la kuchinjia kuku katika machinjio ya kuku iliyojengwa katika kijiji cha Mbande Wilayani Kongwa wakati alipoitembelea Machinjio hiyo. 

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Pauline Gekul ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kujiendesha kibiashara ili iweze kukabiliana na changamoto zinazo ikabili.

Gekul ameyasema hayo  wakati alipo tembelea kituo cha TALIRI na LITA Mpwapwa kwa lengo la kukagua kazi zinazofanywa na taasisi hizo.

Katika taarifa iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TALIRI, Dkt. Jonas Kizima ilielezea changamoto wanazokabiliana nazo zikiwemo za upungufu wa watumishi, uhaba wa vitendea kazi na uhaba wa rasilimali fedha kwa shughuli za kiutafiti. Lakini pia alizungumzia mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto hizo.

Kwa kuwa changamoto nyingi zinahitaji fedha ili kuzitatua ndipo Naibu Waziri Gekul akawaagiza TALIRI kujipanga vizuri ili sasa waweze kujiendesha kibiashara kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutatua changamoto walizonazo badala ya kusubiri kupata fedha kutoka Serikalini.

Pia amewapa miezi mitatu kuhakikisha wanawalipa vibarua wanaochunga ng'ombe pamoja na walinzi mishahara yao ya miezi sita wanayodai.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri amemshukuru Naibu Waziri kwa maamuzi yake ya kitembelea taasisi hizo na kutatua tatizo la mishahara ya vibarua na walinzi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI, Bw. Jonas Kizima amesema wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Naibu Waziri na watakwenda kuyafanyia kazi hasa suala la taasisi hiyo kujiendesha kibiashara.

Katika ziara yake hiyo Wilayani Mpwapwa, pia ametembelea wilaya ya Kongwa ambapo amatembelea Ranchi ya Kongwa, shamba la malisho la mfugaji Bw. Mnyonaki lililopo katika kijiji cha Msunjilile wilayani Kongwa na Machinjio ya kuku iliyopo katika kijiji cha

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...