Kulikua na ghasia wakati wazazi walipoungana na mabinti zaoImage caption: Kulikua na ghasia wakati wazazi walipoungana na mabinti zao
Kulikuwa na tukio la ghasia Jumatano Kaskazini –magharibi mwa Nigeria wakati wazazi walipokuwa wanaungana tena na mabinti zao waliokuwa wametekwa nyara katika mji wa Jangebe.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema watu watatu walipigwa waliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama.
Ufyatulianaji wa risasi uliripotiwa kutokea baada ya wazazi, waliokuwa wamechoshwa na urefu wa hafla ya kuwapokeza watoto wao kuanza kuwarushia mawe maafisa wa serikali.
Wasichana 279 wa shule waliotekwa nyara Ijumaa iliopita, wamekuwa chini ya ulinzi wa serikali tangu walipoachiwa huru siku ya Jumanne.
Mtaalamuwa Umoja wa Mataifa ametoa wito wanafinzi hao wapewe ushauri nasaha haraka iwezekanavyo.
Mama mmoja aliliambia shirika la habari la AFP kwamba walitaka kurudi nyumbani mapema kabla ya giza kuingia kwani njia sio salama.