PAPA Francis atasafiri kwenda Iraq leo Ijumaa katika ziara ya kwanza rasmi nchini humo na safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu kuzuka kwa corona. Safari hiyo ya siku nne inakusudiwa kuihakikishia moyo wa matumaini jamii ya Kikristo inayopungua ya Iraq na kukuza mazungumzo kati ya dini.
Papa atakutana na Kiongozi wa Waislamu wa madhehebu ya Kishia anayeheshimiwa sana, na kufanya sala huko Mosul na kuhudhuria misa katika uwanja wa michezo. Amesisitiza kufanya ziara hiyo licha ya ongezeko jipya la maambukizi ya Covid-19 nchini Iraq na hofu dhidi ya usalama wake.
Saa kadhaa baada ya shambulio la roketi dhidi ya kambi inayokaliwa na wanajeshi wa Marekani siku ya Ijumaa, Papa alisema Wakristo wa Iraq hawawezi "kuvunjwa moyo kwa mara ya pili".
Hii itakuwa ziara ya Papa Francis ya kwanza ya kimataifa kuifanya tangu janga la Covid-19 lilipoanza. Papa John Paul wa pili alifuta mpango wa safari yake nchini humo mwisho wa mwaka 1999 baada ya mazungumzo kati yake na rais wa wakati Iraq wakati huo Saddam Hussein kuvunjika.
Ndani ya miongo miwili tangu wakati huo, moja ya jamii ya zamani ya Wakristo duniani imeshuhudia idadi yake ikipungua kutoka milioni 1.4 hadi karibu 250,000.
Baadhi yao wamekimbilia ughaibuni kwa kuhofia mashambulio kwa misingi ya kidini ambayo yamekumba nchi hiyo tangu Marekani ilipoivamia kijeshi mwaka 2003 na kumuondoa madarakani Saddam.
Maelfu ya watu pia wamefurushwa makwao baada ya wanamgambo wa Islamic State (IS) kuteka eneo la kaskazini mwa Iraq mwaka 2014, na kuharibu makanisa ya kihistoria, kuchukua mali zao na kuwapa masharti ya Julia kodi, kuachana na dini yao ama wauawe.
Papa anatarajia kufanikisha lipi?
Mkuu wa Kanisa Katoliki la Roma analenga kuwatia mayo Wakristo wanaoteswa na kushinikiza amani katika mikutano na viongozi wa kisiasa na kidini, anasema mwandishi wa BBC BBC Mark Lowen, ambaye anafuatilia zira hiyo.
Kanisa kubwa la Grand Immaculate lililopo Qaraqosh liliharibiwa na IS lakini kwa sasa limetengenezwa
Akiwahutubia watu wa Iraq kupitia ujumbe wa video mkesha wa safari yake, Papa Francis alisema "anakuja kama hujaji, masafiri anayetubu, kumuomba Bwana msamaha na upatanisho baada ya miaka kadhaa ya vita na ugaidi, kuomba faraja kutoka kwa Mungu na uponyaji wa mioyo wa majeraha".
Aliongeza: "Nakuja miongoni mwenu pia kama hujaji wa amani…kutafuta ushirika unaotokana na hams ya kuomba pamoja na kutembea pamoja, pia na ndungu na dada zetu wa dini nyingine katika nyayo za Baba Abrahamu , ambaye anajiunga na familia moja ya Waislamu ,Wayahudi na Wakristo."
Papa aliiambia jamii ya Wakristo wa Iraq: "Anataka kuwaletea upendo mzuri wa Kanisa lote ambalo liko karibu na nyinyi na eneo la Mashariki ya kati lillokumbwa na vita, kuhimiza muendelee mbele kwa imani."
Wakristo wa Iraq ni kina nani?
Watu nchini Iraq walikumbatia Ukristo Karne ya kwanza AD. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani , viongozi wa Kikristo wanakadiria kuna Wakristo wachache kuliko 250,000 waliosalia Iraq, baadhi yao – angalau 200,000 – wanaoishi katika Bonde la Ninawi na Mkoa wa Kurdistan kaskazini mwa nchi.
Karibu asilimia 67% kati ya Wakristo hao ni Wakatoliki, ambao wamedumisha utamaduni wao lakini wanatambua mamlaka ya papa mini Roma. Asilimia nyingine 20% ya waumini wa kanisa la Syriac ya Mashariki wanaaminiwa kuwa wa kale nchini Iraq.
Waliosalia Waorthodox wa Syriac, Wakatoliki wa Syriac, Wakatoliki wa Armenian, wengine ni Waanglikana na Waprotestanti.
Ratiba ya Papa itakuwa vipi?
Kutokana na sababu za kiusalama na kuongezeka kwa viwango vya maambukizi ya Covid-19, Papa mwenye umri wa miaka 84- atadhibiti muonekano wake hadharani, mwandishi wetu anasema. Lakini pia kuna hofu ziara hiyo ikawa chanzo cha kuenezwa kwa virusi.
Papa Francis atahudhuria mkutano wa dini mbalimbali kwenye eneo la kale la Ur ambapo anatarajiwa kuwasili mjini Baghdad Ijumaa mchana.