Wednesday, February 17, 2021

Tetesi za soka kimataifa


Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Federico Valverde, 22. (Sun)

Everton itaanza tena juhudi zake za kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 25, msimu huu. (Mail)

Beki wa kati wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car, 24, anasema alikataa ofa ya Liverpool mnamo mwezi Januari wakati wa uhamisho. (Goal)

Mlinzi wa Austria David Alaba, 28, anataka Real Madrid kuwa klabu yake itakayofuata baada ya Bayern Munich mwisho wa msimu pia ameanza kujifunza Kihispania - lakini hatua ya kuhamia Bernabeu inategemea hatma ya beki wa kati wa Real raia wa Uhispania Ramos. (Mirror)

Alaba bado ndio mlengwa mkuu wa Real kama mbadala wa Ramos, 34, ingawa mlinzi wa RB Leipzig na Bayern Munich - raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 22, alikuwa ndiye wanayemtaka. (AS - in Spanish)

Manchester United ilikaribia kumsajili Upamecano kwa pauni milioni 1.9 mwaka 2015, kulingana na mshauri wa mchezaji huyo. (Mirror)

Kumpiga kalamu kocha wa Ureno Jose Mourinho kutaigharimu Tottenham takriban euro milioni 40. (A Bola - in Portuguese)

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann na kocha wa Leicester Brendan Rodgers huenda wakachukua nafasi ya Mourinho huko Tottenham. (Mail)

Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy awali alijaribu kumchukua aliyekuwa kocha Liverpool na Celtic Rodgers katika klabu yake na huenda akaanza tena jitihada hizo ikiwa Mourinho ataondoka. (Eurosport)

Winga wa Uingereza Demarai Gray, 24, anasema hakupewa mkataba mpya na Leicester kabla hajahamia Bayer Leverkusen mnamo mwezi Januari. (Sky Sports)

Baada ya kuendeleza mkataba wa mshambuliaji Mason Greenwood, 19, Manchester United huenda ikaweka kipaumbele katika kumsajili beki wa kati mpya au mshambuliaji wa Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland, 20, juu ya uhamisho wa mchezaji wa Dortmund Jadon Sancho, 20. (Express)

Manchester United iko tayari kutoa ofa ya euro milioni 70 kuipiku Real Madrid na Paris St-Germain katika usajili wa mlinzi wa Sevilla Jules Kounde, 22. (TeamTalk)

Real Madrid imeungana na wengine wanaotaka kumsajili beki wa kati wa Braga raia wa Ureno David Carmo. Liverpool ilijaribu kumsajili mchezaji huyo, 21, mnamo mwezi Januari lakini mazungumzo yao hayakufanikiwa kuzaa matunda. (AS - in Spanish)

Arsenal ina uwezekano mkubwa wa kutoa ofa kwa David Luiz, 33, kwa kuendeleza mkataba wake ikiwa mchezaji huyo wa Brazil atakubali kuwa mchezaji na kufunza wengine. (Football.London)

Newcastle haijaribu kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa England Daniel Sturridge kwa uhamisho wa bure licha ya tetesi hizo. Mchezaji huyo, 31, sasa yuko huru. (Football Insider)

Na kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema hakuna mazungumzo ambayo yamefanyika kuhusiana na hatma yake Old Trafford, mkataba wake ukiwa unamalizika mwisho wa msimu ujao. (Mirror)
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...