Tuesday, February 2, 2021

Miko Sonko kufikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za ghasia





Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani, huku wapelelezi wakitaka kupata muda zaidi kumuwajibisha juu ya madai ya kuhusika kwake katika ghasia za uchaguzi wa mwaka 2017 nchini Kenya.
Hivi karibuni Bw Sonko alidai kwamba yeye na katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Karanja Kibicho alihusika katika kupanga ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa mzozo wa matokeo ya uchaguzi.

Jumatatu gavana huyo wa zamani alijiwasilisha binafsi katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka ya umma (DCI) baada ya kutaka agizo la mahakama la kumzuia kushitakiwa bila mafanikio.

Wakili wake,John Khaminwa, alisema Mahakama ya juu ilitupilia mbali ombi kutaka mahakama isitishe kesi yake , na kumlazimisha Bw Sonko kujisalimisha katika makao makuu ya DCI.

Sonko alitaka mahakama itoe agizo lake dhidi ya uamuzi wa Naibu Inspekta mkuu wa polisi na Mkuu wa upelelezi wa DCI John Kariuki wa kumtaka arekodi taarifa kuhusiana na ghasia alizodai kuzifanya katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2017.

Katika ombi lake, Sonko alidai kwamba kuitwa kwake na DCI kulikua ni njama za kutaka akamatwe na polisi.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...