Saturday, February 13, 2021

Namungo Yawekwa Karantini Angola




MSAFARA wa watu 32 wa Klabu ya Namungo ya Tanzania umezuiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Luanda nchini Angola baada ya mamlaka za nchi hiyo kudai kuwa wachezaji watatu na kiongozi mmoja wamepimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

 

 

Mpaka tunaenda hewani, timu ilikuwa bado ipo uwanja wa ndege huku utata ukitawala kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutaka msafara mzima ama urudi Tanzania au uwekwe karantini. Lakini mwisho wa siku imeamriwa msafara mzima wa klabu hiyo kuweka karantini kwa siku tatu.

 

 

Namungo ipo Angola kuchuana na Clube Desportivo 1ยบ de Agosto katika mechi ya Kombe la Shirikisho ambayo ilipangwa kupigwa kesho Jumapili, Februari 14.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...