Na Omary Mngindo, Ruvu
CHAMA Cha Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) kimeishukuru Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini TADB, kwa kuusaidia ushirika huo kwa kuukopesha dhana za kilimo kuanzia matrekta, mbolea na pembejeo.
Aidha katika mkopo huo wa shilingi milioni 480, uliogawanyika maeneo mawili ambayo ni upatikanaji wa matrekta mawili yenye ukubwa wa pawa 75, majembe na Oktaveta, huku wa pili ukiwa ni wa mbegu tani 34, na mbolea tani 2,700 zitazotosha kwa msimu mzima wa kilimo kwa wanachama hao, wakiwemo waliopo nje ya ushirika lengo kuu la benki ni kuona kilimo kinakuwa chenye tija.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa ushirika huo Sadala Chacha, akizungumza na Waandishi wa habari katika mashamba hayo yaliyopo Kitongoji cha Chauru, Kijiji cha Visezi, halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Pwani, ambapo alisema kuwa benki hiyo imewakopesha kiasi cha shilingi milioni 480 zilizogawanyika kwenye makundi hayo.
"Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 tumepokea mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 480 uliogawanyika sehemu mbili, kwanza zana za kilimo ambapo tumepata matrekta mawili yenye uwezo wa pawa 75, mbolea pamoja na pembejeo tutazowakopesha wanachama wetu, wataorejezha baada ya mavuno, kwakuwa benki inadhamilia kuinua kilimo hata walio nje ya ushirika wanakaribishwa kuja kununua kwa pesa tasilimu," alisema Chacha.
Aliongeza kwamba msimu wa mwaka 2020/2021 wamepokea mbolea tani 2,700 na mbegu tani 34 kutoka benki hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye msimu huo, na kwamba taratibu zote zimekamilika ikiwemo kuanza kulima mashamba ya wanachama hao wataozipata kwa mkopo, kisha kulipa baada ya mavuno.
Kwa upande wake ofisa kilimo wa ushirika huo alisema kuwa Dawson Daniel alisema kuwa wameshaanza kulima mashamba yao, huku akieleza kwamba katika ushirika huo mashamba yote yanalimwa kitaalamu, na kwamba kuna wataalamu wa kila sekta, na kuwa kwa msimu huu wa wanataraji kuvuka lengo la msimu uliopita.
Meneja wa CHAURU Victoria Olotu aliwaambia waandishi kuwa kutokana na kupatikana mapema kwa mbolea aina ya yaramila otesha tani 2700 ya kulimia na kupandia kutoka na mbegu tani 28 kutoka tali, zitakuwa na manufa makubwa wakulima wanachama na walio nje ya ushirika huo.
"Kupatikanaji kwa mbegu na mbolea kwa wakati kutasaidia wakulima kuwa na uhakika wa mavuno, kwani wanazinunua hapahapa tofauti nanawali walizipata kwa walanguzi mitaani kwa bei kati ya sh. 65,000 mpaka 67,000, hapa watazipata kwa sh. 60,000, mbegu ya kukuzia tunauza kwa sh. 59,000 wakati mitaani zinauzwa sh. 63,000 mpaka 64,000 wafike ofisini" alisema Olotu.
Kwa upande wao wakulima Abdallah Mbagu na Magreth Elias walisema kuwa kwa mwaka huu wa kilimo wanataraji kunufaika zaidi kutokana na maandalizi ya mapema katika kuelekea msimu huo, huku Magreth akiwataka wanawake kuchangamkia kilimo, huku Abdalah akitoa wito kwa vijana kuacha kukaa vijiweni badala yake wajiunge na ilimo.