Na Timothy Itembe Mara.
Mbunge wa Tarime vijijini,Mwita Mwikwabe Waitara alisema kilichokwamisha madiwani wa halmashauri ya Tarime vijijin kuchelewa kuapishwa kuwa ni makundi ya koo.
"Kutajwa kila mara mgawanyiko wa koo katika kabila la Wakura wilayani Tarime ni moja ya sababu ambayo inaninyima usingizi kila kukicha na ni swala ambalo linatakiwa kupigwa vita"lisema Waitara.
Mgawanyiko wa koo ndani ya kabila la Wakurya katika halmashauri ya Tarime kulisababisha mchakato wa kuapishwa madiwani kuchelewa pale ambapo mgawanyo wa viti maalumu uliingia kasoro liongeza kusema.
Waitara ambaye pia ni Naibi waziri muungano na Mazingira alisema baada yamgawanyo huo wa viti maalumu kuwa na kasoro ilimpidi kuingilia kati kwa maana koo ya Watimbaru hawakuwa wamepata kiti cha viti maalumu licha ya kuwa wanakata taklibani 5 ndani ya halmashauri hiyo.
Naibu Waziri aliongeza kusema baada ya changamoto hiyo kutatuliwa madiwani waliaapishwa chini ya Hakimu mkazi (11)wa mahakama ya Mwanzo Nyamwaga,Adeline Kashushura ambapo walitakiwa kulinda viapo vyao.
Wakati huo huo madiwani hao walipokea kiapo cha ahadi ya maadili ili kusimamia misingi ya viongozi wa umma,misingi ya katiba ambayo nisheria iliyoainishwa katika kanuni za madiwani.
Naye diwani kata ya Matongo,Godfrey Kegoye alisema baada ya kula kiapo alisema atahakikisha anawaletea wananchi wake maendeleo yaliyokuwa yamekwama baada ya kata hiyo hapo nyuma ilikuwa inaongozwa na upinzani na sasa ipo chini ya CCM.
Kegoye aliongeza kusema moja ya miradi ambayo ataanza nayo ni pamoja na miradi ya maji,miundombinu ya Barabara,Elimu Afya ikiwewmo ujenzi wa chuo cha VETA ili vijana kusoma na kuongeza ujuzi kwa lengo la kupata ajira mbalimbali.
Kegoye aliongeza kusema kuwa maandalizi ya ujenzi wa Chuo cha veta yamekamilika ikiwemo kupata eneo la ujenzi kwa ajili ya chuo hicho pamoja na wananchi kuchangia shuguli mbalimbali ili kufanikisha.
Mmoja wa wananchi wa jimbo la Tarime vijijini,Perry Magitta alisema jimbo hilo lilikuwa chini ya upinzani lakini sasa linaongozwa na CCM kwa hali hiyo wananchi wategemee maendeleo.
Wananchi kwasababu ya kumwamini Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli waliamua kutoa kura kwa Chama cha mapinduzi ili wanufaike na maendeleo badala ya kuendelea kuunga juhudi za upinzani waliokuwa wakipinga kila jambo hata kama lilikuwa jema na la maendeleo.
Magitta alimaliza kwa kusema kuwa moja ya sababu iliyowaangusha wapinzani kwenye mchakato wa uchaguzi 2020 ilikuwa ile ya kususia vikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Bajeti ikipitishwa na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Kwa upande wa mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijini,Apoll Tindwa aliwashukuru madiwani kupokea kiapo ambapo aliwaahidi kutoa ushirikiano kwa watumishi ili kuiletea maendeleo halmashauri hiyo.
Source