Mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda imeandikia Google, jukwaa la kushirikisha video, kuomba ifunge vituo 14 vinavyodaiwa kuhusishwa na ghasia za mwezi uliopita ambazo zilisababisha zaidi ya watu 50 kufa.
Ghasia zilizuka katika mji mkuu wa Kampala na miji mingine mikuu kufuatia kukamatwa kwa mgombea wa urais wa upinzani na mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kwa kukiuka masharti ya kudhibiti ugonjwa corona.
Baadhi ya vituo vya YouTube vinavyohusishwa na Bobi Wine ndivyo vinalengwa, lakini mkuu wa masuala ya sheria wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda ameambia kituo cha televisheni cha Bloomberg kwamba ni "bahati mbaya" tu.
Katika barua yake kwa Google,Tume hiyo ilisema vituo hivyo vilitumiwa kuchochea virugu na vinatangaza maudhui yanayokiuka sheria, Gazeti la Daily Monitor linaripoti.
Raia wa Uganda wanajianda kushiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge Januari 14. Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu, inataka kuchaguliwa tena.
Media hizo ni.
Ghetto TV
Map Mediya
Busesa Media Updates
Uganda Empya
KK TV Uganda
Ekyooto TV
Bobi Wine 2021
Namungo Media
JB Muwonge
TMO Online
Lumbuye Fred
Trending Channel Ug
Uganda Yaffe
Uganda News Update
Source