Wednesday, December 30, 2020

Tetemeko kubwa la ardhi lawaua watu sita Croatia


Juhudi za kuwatafuta wahanga zimeendelea usiku kucha wa leo, baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 kwa vipimo vya Richter kuyapiga maeneo ya katikati mwa Croatia na kusababisha vifo vya watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Timu ya uokoaji ilikuwa ikiwaondoa watu kutoka kwenye kifusi cha majengo yaliyoporomoka katika mji wa Petrinja, huku wanajeshi wakiwasili eneo la tukio kwa ajili ya usaidizi. 

Tetemeko hilo pia limesikika katika mji mkuu wa Croatia wa Zagreb na katika mji mkuu wa Austria wa Vienna. Hilo linakuwa tetemeko la pili kutokea katika eneo hilo ndani ya siku mbili. 

Marundo ya mawe, matofali na vigae vimeonekana kutapakaa katika mitaa ya Petrinja, baada ya tetemeko na magari yaliyokuwa yameegeshwa barabarani yalikuwa yamevunjwa na vifusi vinavyoanguka.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...