Nyota wa Liverpool azua gumzo lililotanda chuki miongoni mwa mashabiki wake mitandaoni baada ya kuweka picha zinazoonesha ujumbe wa kusherehekea krismasi.
Mashabiki wa mshabuliaji huyo wa Liverpool na Misri Mohamed Salah wameandika ujumbe wa chuki kuonesha kutofurahishwa na kitendo chake kama nyota wa Kiislamu kutuma ujumbe wa krismasi akiwa pamoja na familia yake.
Salah, 28, aliweka picha mtandaoni zinazomuonesha yeye na familia yake wakiwa wamevalia vizuri na kusimama mbele ya mti wa Krismasi, na kwenye ujumbe huo akaweka emoji 2, na hashtag Merry Christmas.
Ujumbe wa Salah kwenye mtandao wa Instagram umepata 'likes' zaidi ya millioni 2.3 huku ujumbe wake kwenye Twitter wenye picha hizo hizo ukiwa na 'likes' zaidi ya 300,000.
Lakini pia ujumbe huo wa Salah umesababisha hasira kwa baadhi ya wafuasi wake Waislamu ambao wamehoji kuwa nyota huyo wa Kiislamu haruhusiwi kusherekea sikukuu ya Krismasi.
Moja ya jumbe zilizojibu ule wa Salah umeandikwa:
"Kama Muislamu hatustahili kusherehekea au hata kupongeza dini zingine wakati wanasherehe zao''.
Shabiki mwingine akamjibu:
"Hii ndio sababu [Nyota wa Arsenal na Misri] Mohammed Elneny ndio mfalme wa Misri na sio wewe"
Wengine walioghadhabishwa na hatua ya Mo Salah ni kama ifuatavyo: