Sunday, December 20, 2020

Mike Sonko, Gavana Tozi Aliyetumbuliwa




Mike Gidion Kioko Mbuvi Sonko, kama alivyojulikana na wengi, hakuwa Gavana wako wa kawaida. Tofauti na wanasiasa wengi wanaojulikana kwa kuvaa suti za bei ghali, Sonko, mwenye umri wa miaka 45, alikuwa na ujana ndani yake.

Bunge la Seneti nchini Kenya limepiga kura kumuondoa Mike Mubuvi Sonko kama gavana wa Nairobi , katika hatua ambayo imekomesha miaka mitatu ya utawala wake uliogubikwa na utata.Sonko anatuhumiwa kwa uvunjaji wa katiba, matumizi mbaya wa mamlaka , utovu wa nidhamu, na uhalifu.

 

Mara kwa mara Sonko alionekana katika maeneo ya umma akiwa amevalia mavazi ya wanamitindo wa Marekani kama vile Gucci na Louis Vuitton.



Sonko ni maarufu sana kwa kuvaa vito vya thamani. Anajulikana sana kwa kuvaa vito vya thamani; pete na bangili nyingi za dhahabu, ambavyo vinaja hasa wa Nairobi huviita 'bling bling'.

 

Sonko alipata umaarufu mkubwa alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kama Mbunge wa eneo bunge la Makadara jijini Nairobi. Mara moja alianza kuonekana katika maeneo ya umma akisambaza pesa kwa watu maskini hususan katika maeneo ya nyumba za za vibanda.

 

Umaarufu wake uliendelea kupanda zaidi na zaidi baada ya kwenda katika mitaa ya mabanda ya Mukuru, na kulaƂa nje usiku kucha na wakazi wa huko waliokuwa wamebomolewa nyumba zao na serikali. Mike Sonko amekuwa kipenzi cha watu hasa masikini hasa kwa kuwa amekuwa akiwapatia misaada.

 

Sonko alianzisha mradi wake maarufu kama 'Sonko Rescue Team' ambao uliwasaidia wakazi wa mitaa ya mabanda wakati wa harusi, kutoa magari ya kusafirisha miili ya wapendwa wao waliofariki, magari ya zima moto, ambilansi na hata kusafisha maeneo kadhaa jiji la Nairobi.



Lakini kando na hayo mazuri, Gavana Sonko atakumbukwa kwa rekodi ya uhalifu. Idara ya magereza nchini Kenya inasema Sonko alitoroka gerezani takriban miaka 20 iliyopita. Ni madai ambayo Sonko mwenyewe aliyathibitisha katika mahojiano ya Televisheni nchini Kenya.

 

Mwaka jana Sonko pia alikamatwa kwa tuhuma za ufisadi, japo amesisitiza kuwa tuhuma hizo zilikuwa njama za wapinzani wake kisiasa.

 

Gavana aliyetumia lugha chafu. Sonko anakumbukwa sana kwa kutumia lugha chafu, na maneno yasiyoweza kuchapishwa, hususan wakati alipokuwa akilumbana na wapinzani wake


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...